Hili ni daraja linalohusisha madaraja mawili pacha yaliyojengwa kwa zege huko Lousiana Marekani. Daraja hili linakatiza ziwa Pontchartrain na lina urefu wa kilometa 36.69.
Runyang ni daraja kubwa linalokatiza mto Yangtze katika jimbo la Jiangsu huko China. Daraja hili lina urefu wa kilometa 35.66 na linaunganisha sehemu ya kusini ya Zhenjiang na ya kaskazini ya Yangzhou mwa mto Yangtze. Daraja hili ni sehemu ya njia ya mwendokasi ya Beijing-Shanghai.
Daraja la Donghai ni moja kati ya madaraja marefu zaidi duniani yanayokatiza bahari. Daraja hili lina urefu wa kilometa 32.5 na linaunganisha Shanghai na bandari ya kina kirefu ya Yangshan huko China.
Hili ni daraja la treni ya juu linalotoka katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Pudong hadi kwenye viunga vya pembezoni vya mji wa Shanghai huko China.
Njia hii huwafikisha wasafiri mahali ambapo wanaweza kupata usafiri wa chini ya ardhi wa kuelekea watakako. Daraja hili lina urefu wa kilometa 29.9
Atchafalaya ni daraja linalopatikana huko nchini Marekani na lina urefu wa kilometa 29.29. Atchafalaya ni daraja la tatu kwa urefu huko nchini Marekani na la 14 duniani.
Hili ni daraja linalopatikana katika jimbo la Shandong huko China likiwa na urefu wa kilometa 26.7. Mnamo mwezi Disemba mwaka 2012 daraja la Jiaozhou liwekwa kwenye rekodi za dunia za madaraja marefu zaidi yaliyoko juu ya maji.
Hili ni daraja linalopatikana katika jimbo la Shandong huko China likiwa na urefu wa kilometa 26.7. Mnamo mwezi Disemba mwaka 2012 daraja la Jiaozhou liwekwa kwenye rekodi za dunia za madaraja marefu zaidi yaliyoko juu ya maji.
Kwa hakika kuna madaraja mengi zaidi ya haya, lakini nimekuorodheshea haya 15 marefu na makubwa zaidi duniani. Naamini umejifunza mengi pamoja na kufurahia makala hii.
Unaweza ukawa unajiuliza tovuti hizo ni zipi? Intaneti imejaa tovuti nyingi sana, za maana na zisizo za maana. Hata hivyo bado tovuti za maana na zenye manufaa zimeweza kujibainisha wazi kati ya zile zisizofaa.
Hii ni tovuti nzuri sana kwa ajili ya kukagua kama barua pepe yako imeshavuja kwenye taarifa za siri zilizoibiwa. Hivi leo kuna makampuni na tovuti nyingi zinazodukuliwa na kuibiwa taarifa za watumiaji wake. Hivyo unaweza kuwa ni moja kati ya watu ambao barua pepe zao ziliibiwa. Ikiwa utaambiwa kua barua pepe yako imeonekana kwenye taarifa zilizodukuliwa basi badili neno la siri haraka.
Tovuti hii inafaa ikiwa unahitaji barua pepe ya muda mfupi tu. Inawezekana unataka kuingia kwenye tovuti fulani lakini inataka uweke barua pepe yako; ikiwa hautaki kuweka barua pepe yako halisi basi unaweza kupata barua pepe ya muda katika tovuti hii.
Kuna watu wanaopenda kufanyia kazi kwenye mazingira yenye sauti fulani ndipo wafanye kazi vizuri. Ikiwa wewe ni mmoja wapo Noisli ina sauti kama vile kutiririka kwa maji na sauti za ndege, hivyo kukuwezesha kufanya kazi katika mazingira unayoyapenda.
Deadmansswitch ni tovuti ambayo hukuwezesha kutuma barua pepe baada ya kufariki. Kutuma barua pepe baada ya kufariki?
Ndiyo; tovuti hii itakutumia barua pepe kila baada ya kipindi fulani cha muda kuona kama bado upo hai, ikiwa itabaini kuwa haupo hai basi itatuma barua pepe kwa watu uliowachagua.
Hii inafaa sana pale ambapo kuna taarifa ambazo ungependa kuzitoa baada ya wewe kufa kama vile wosia, tarifa zako za kibenki, mali zako, wadaiwa wako n.k
Smallpdf ni tovuti ni tovuti itakayokusaidia kwa mahitaji yako yote yanayohusiana na pdf. Ikiwa unataka kutengeneza, kuhariri au kubadili mafaili ya pdf basi hii tovuti ni kwa ajili yako.