Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Maana za maneno

Je unasumbuka kubeba kamusi ya Kiingereza kila unapokuwa? Ukiwa na Google huhitaji kubeba kamusi kwani unaweza kupata maana za maneno yote kupitia Google. Unachotakiwa kufanya ni kuandika “Dictionary” kwenye Google kisha utapata dictionary unayoweza kuitumia kutafuta maneno mbalimbali. Unaweza pia kuandika “define your_word” na utapata maana ya neno uliloliandika.
 
Tafsiri

Unaweza kutafsiri maneno kutoka lugha moja hadi nyingine kwa urahisi na bure kabisa uwapo na Google.

Unaweza pia kusoma maandishi kwa sauti kupitia Google; kwa mfano ikiwa unataka kusikiliza andiko fulani badala ya kulisoma basi unaweza kutumia Google translate.

Unachotakiwa kufanya ni kutafuta “translate” kwenye Google kisha utapata ukurasa unaoweza kuweka maandishi yako pamoja na kuchagua lugha.
 
Kubadilisha vipimo

Je huwa unahitaji kubadili vipimo mbalimbali? Unaweza kubadili vipimo mbalimbali kwa kutumia Google. Kwa kutafuta “unit converter” utapata ukurasa wenye kukuwezesha kubadilisha vipimo mbalimbali.
 
Viwango vya kubadilisha fedha

Je umekuwa ukipata shida kufahamu viwango vya kubadilisha fedha mbalimbali duniani?

Usihangaike tena, unaweza kuandika “currency convertor” kwenye Google na mara moja utapata ukurasa kwa ajili ya kufahamu viwango vya kubadilishia fedha.
 
Kihesabu muda

Unaweza kupata kihesabu muda (timer and stopwatch) kizuri kitakachokusaidia katika shughuli mbalimbali kwa kutumia Google. Unachotakiwa kufanya ni kutafuta neno “timer” kisha uweke muda unaotaka kuhesabu na ubonyeze start.
 
Hali ya hewa

Hakuna haja ya kukaa kusubiri tena habari za hali ya hewa. Kwa kutumia Google, unaweza kufahamu hali ya hewa ya miji na maeneo mbalimbali duniani.

Kwa mfano unaweza kutafuta “Weather Kampala” au “Weather Arusha” na utapata taarifa kamili.
 
Kufahamu kurasa za tovuti fulani zilizoko kwenye Google

Ikiwa unataka kufahamu ni kurasa ngapi na zipi zimeorodheshwa au kutambulika (indexed) na Google katika tovuti fulani, unaweza kuandika “site:mfano.com” na utaona kurasa za tovuti yako.

Huduma hii ya Google ni muhimu sana kwa wenye tovuti na blogs kwani wataitumia kubaini ni kurasa zipi ambazo tayari Google imeshazitambua kutoka kwenye tovuti au blog zao.
 
Naamini sasa umekubaliana na mimi kuwa Google ni rafiki yetu bora na wa karibu sana. Ni wazi kuwa yapo mambo mengi sana unayoweza kuyafanya kwa kutumia Google, lakini mimi nimeorodhesha 10 tu. Je wewe huwa unatumia Google kwa mambo haya? Je kuna mambo mengine ambayo wewe unayafanya kwenye Google?
 
Tunakukumbuka,
Mwenyezi Mungu akulaze mahali pema
FB_IMG_1563254365099.jpeg
 
Back
Top Bottom