Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Aidha, andiko la Wesley Gilbert linalosomeka Our Man in Zanzibar. Andiko hili linaeleza kwa uchambuzi mkubwa jinsi Marekani ikiwa dola ya kwanza ya kigeni, ilivyoanzisha ubalozi wake Zanzibar mwaka 1835 na kuteua Balozi wake wa mwanzo mfanyabiashara Bwana Richard Waters aliyetokea Salem, Massachusetts na jinsi Kijiji cha Selemu, Unguja kilivyopata jina hilo kutoka kwa Balozi huyu.
 
Kubwa zaidi, inaeleza biashara kubwa iliyokuwa ikifanyika baina ya Zanzibar na Marekani hadi kuwashitua Waingereza ambao walimtuma Captain Hart kutoka Bombay kuja Zanzibar kuchunguza urafiki wa Marekani na Zanzibar. Waingereza nao wakalazimika kuingia Mkataba wa urafiki na Zanzibar miaka miwili baadaye.
Suala la msingi hapa hivi kuna uhusiano gani wa hadithi nilizotangulia kuzieleza na msingi wa makala hii?
 
Badala yake juhudi kubwa zinafanyika kufuta hilo. Ukiuliza hakuna mwenye majibu ya vita hivi vya kupambana na fahari hii ya Zanzibar. Kinachotia moyo, tena sana, ni ule muamko wa watu wengi wa Zanzibar na muungano wa hisia zao za kulinda kwa Imani yao ya dhati fahari na utukufu wa nchi yao.
 
Pili, Zanzibar ina mustakbala wake ambao upo majaribuni. Mustakbala sio wa kizazi cha leo bali vizazi vijavyo. Bila ya kuwa na maamuzi juu ya mustakbala wao na bila ya kuwa na kauli juu ya mustakbala wao, hawatafaidi maendeleo ya makubwa ya dunia katika nyanja mbali mbali. Kwa mfano hili la maendeleo ya teknonolojia. Zanzibar ina vijana waliotapakaa dunia nzima wenye vipawa vya aina yake katika fani ya teknolojia.
 
Na naam, likaingizwa katika Orodha ya Muungano. Nilipopata fursa ya kuwafafanulia hatari ya jambo hilo kuwa la Muungano, pamoja na wao kukubali hatari hiyo, lakini ushauri ulipita sikio la kulia ukatokea la kushoto [au kinyume chake]. Mawasiliano ndio uchumi wa dunia tunakoelekea. Ndio maisha. Afya, usafiri, kilimo, elimu, huduma za fedha zote zitategemea mawasiliano. Unawezaje kutoa nyenzo hiyo muhimu tena bila kuweka ufafanuzi wala mipaka.?
 
Unaposikia mmoja akianza kusema Machotara na Wahindi si kwao Zanzibar inashangaza. Inabidi umkumbushe tu mambo matatu kwa haraka labda atarudi katika mstari:
  1. Mosi, kwamba mji wa Chake Chake wa awali kabisa ambao hadi mwaka 1914 ulikuwa na nyumba karibu 200 ulijengwa katika ardhi iliyotolewa Wakfu na bwana mmoja wa kiarabu Bwana Nassor bin Khalef mwaka 1825 hata kabla Sultani hajahamia Zanzibar.
  2. Pili, kwamba nyumba ya kwanza iliyotaifishwa Zanzibar mwaka 1964 kupitia Legal Notice No. 5 la 1964 ilijengwa na Tayabhali Karimjee kwa matumizi yake binafsi na hadi leo ipo pale Migombani na ndio makazi rasmi ya Serikali.
  3. Tatu, kwamba wengi wanaojifanya ndio wenye Zanzibar ya leo, wazazi wao au wao wenyewe waliomba uraia wa Zanzibar mwaka 1961 na 1962. Orodha ya majina yao ipo katika magazeti rasmi ya Serikali ya miaka hiyo.
 
Dhamira ya dhati yahitajika
Katika hali hiyo, Zanzibar inahitaji dhamira ya dhati kabisa ya kuunganishwa. Dhamira ya kuondoa hisia ya kuwa kuna wenye Zanzibar na wengine wapo kwa ihsani ya wenye Zanzibar ambao hawaonekani kuwa na ihsani. Dhamira ya kujenga misingi ya umoja inayoendana na uhalisia uliopo kwamba Wazanzibari ni wamoja.
 
Wengi wa Wazanzibari wa leo wanalijua hilo na wana hamu na hilo. Wanahitaji viongozi wenye dhamira ya kweli, wenye maono na wanaoamini katika hilo. Viongozi ambao wanatambua umoja wa Wazanzibari haugombani hata kidogo na umoja na mshikamano wa Watanzania wasiokerwa na maendeleo ya Zanzibar na waoamini kwamba maendeleo ya Zanzibar ni faida kwa Tanzania yote.
 
Ndio maana, nikasema Maalim Seif una mkate gaeni, usiuache ukaungua. Matarajio ya Wazanzibari katika hayo niliyoyaeleza ndio mkate wenyewe. Imani yao kwa kiongozi anayeweza kusimamia matarajio hayo ndio yatayoamua siasa na mustakbala wa Zanzibar. Sio sura, sio rangi, siyo bendera, siyo nguvu wala chama.
 
Lakini kutafuta, kudai na kusimamia jema, siku zote kuna dhoruba, maafa na mikiki, wakati mwengine ya kukatisha tamaa kabisa. Kama kutafuta jema ni rahisi, basi ingekuwa rahisi kazi ya Mitume wa Mungu, maana waliteuliwa na Mungu kusimamia kazi ya Mungu.

Hata hivyo walikutana na dhoruba, mpaka baadhi ya wakati ikabidi Mungu mwenyewe awaliwaze na kuwapa moyo. Waswahili wana msemo “Mpishi ndiye Apyaye”. Lakini kovu za kuungua huko katika upishi wa jema ndiyo nuru, ndio haiba, ndio heshima na ndio kito cha ufalme wa kila mtafuta jema.
 
Jeuri ya Z’bar kutaka kuanzisha benki kuu ilivyozimwa
RAIS Abeid Amani Karume wa Zanzibar, siku zote hakufurahia muundo wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar (baadaye ukaitwa Tanzania) ulivyokuwa, tangu ulipoanzishwa, Aprili 26, 1964 hadi kifo chake, Aprili 7, 1972 akidai kwamba ni “koti” lililombana na alitamani daima kulivua.

Kwa sababu hii alihakikisha kwamba, Muungano haumpunguzii madaraka yake Visiwani; aliiongoza Zanzibar kama “nchi huru” hata kwa mambo ambayo yalikuwa ya Muungano sawa na kwamba juhudi zake za kujiimarisha kimadaraka zilikuwa ni kutafuta “uhuru” wa Zanzibar nje ya Muungano.
 
Karume hakujali mgawanyo wa mamlaka na madaraka kati ya yale ya Muungano na yale ya Zanzibar. Ukiacha mambo ya Nje, Zanzibar iliendelea kudhibiti kivyake madaraka na mambo yote juu ya Uhamiaji, Biashara ya Nje na Mikopo, Utumishi wa Umma, Bandari, Posta na Simu, Jeshi na Usalama wa Taifa ambayo vinginevyo yalipashwa kusimamiwa na Serikali ya Muungano.

Na kwa chukizo kwa Nyerere, alitangaza kuwa asingeruhusu uchaguzi kufanyika Visiwani kwa miaka 50; akatangaza ukuu (supremacy) wa Chama cha Afro Shirazi (ASP) kuwa juu ya taasisi zote, ikiwamo Katiba ya Jamhuri ya Muungano na taasisi zake.
 
Kana kwamba alikuwa akiimarisha Taifa huru la Zanzibar nje ya Muungano, Amri yake (Decree) juu ya ukuu wa ASP ilianzisha Idara za Jeshi, Usalama wa Taifa (la Zanzibar), Polisi, Vijana, kina mama wa ASP ili kwamba mambo hayo yashughulikiwe kiserikali chini ya idara husika nje ya Muungano.

Kufikia mwaka 1971, Vyeo kama “Rais wa Zanzibar” (chenye kutambuliwa na Katiba ya Muungano), Mawaziri na Manaibu Mawaziri, vilibadilishwa kuitwa “Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi” (badala ya Rais), Mawaziri na Manaibu Mawaziri wakaitwa Wenyeviti na Manaibu Wenyeviti wa Idara; yote haya ilikuwa ni chenga kimamlaka kufanya Katiba ya Muungano isiwe na pa kushika kiutawala Visiwani.
 
Kufikia hapo, ASP kilikuwa ndiyo Serikali na Serikali ilikuwa ndio ASP wakati ikifahamika kwamba, Vyama vya Siasa (ASP na TANU) havikuwa jambo la Muungano. Ikumbukwe kwamba, wakati huo Zanzibar haikuwa na Katiba ambapo ilitawaliwa kwa Amri (Decrees) za Rais zisizohojika.

Na vivyo hivyo, Jamhuri ya Muungano ilitawaliwa na kuongozwa kwa Katiba ya Mpito (Interim Constitution) ambayo ilimpa madaraka Rais wa Jamhuri ya Muungano, kuifanyia marekebisho kadri alivyoona inafaa katika kipindi cha mpito cha mwaka mmoja kuelekea Katiba ya kudumu, isipokuwa kwa mambo kumi na moja ya Muungano (kutopunguza au kuongeza) yenye kulindwa na Mkataba wa Muungano (Articles of Union), uliotiwa sahihi na waasisi wake, Aprili 22, 1964.

Kitendo cha Karume kuendelea kudhibiti baadhi ya mambo ya Muungano Visiwani, kilitafsiriwa kuwa cha mabavu na “usaliti” kwa Muungano.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…