Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

FB_IMG_1561592294323.jpeg
 
Miaka ile tulikuwa tunawaokota ndalala, miteja, mwaka, ruvuma, madenge, pazi, si unakumbuka zile taa za mitaani wakati ule.
Tulifika mpaka mombo, boko, wailes tukiwasaka saa 12 mpka 2 za usiku.
Daaaa utoto kazi mkuu[emoji23][emoji23]
Nakumbuka enzi hizo walipatikana sana maeneo ya Chuo cha bandari(Tmk),Tandika maghorofani,Karakana(Tzr) na Yombo mashambani, tulikuwa tunang'ang'aniana na nyoka, mijusi, vyura... Utoto raha sana
 
Maalim Seif una mkate gaeni
aliandika muheshimiwa othman massoud

Leo nimetafuta muda nikasoma kwa kituo taarifa iliyochapishwa hivi karibuni na Shirika la Umoja wa Mataifa linalosimamia tasnia ya ubunifu na uvumbuzi linaloitwa kwa Kiingereza World Intellectual Property Organisation [WIPO] inayohusu maendeleo ya teknolojia katika upande wa Artificial Intelligence [kwa hakika nimeshindwa kupata tafsiri yake sahihi ya Kiswahili]. Hata hivyo kwa kifupi ni jinsi mashine zinavyoweza kufanya kazi ya kutumia “akili” ya kikomputa. Wenyewe wanasema huu sasa ndio umeme wa karne ya 21.
 
Kwa kutumia “akili” hiyo, mashine zinaweza sasa kusoma maandishi ya mkono, kutafsiri lugha moja kwenda nyengine na mambo mengine kadhaa ambayo ni ya ajabu kwa kweli. Kilichonivuta hisia ni kwamba taasisi za taaluma za China zinaongoza katika taaluma hii. Naam China hii ambayo nchini kwetu tunadhani tunafafanana nayo kisiasa. Tunayodhani bado inasimama katika uono wa miaka ile ya China yetu sisi Afrika.
 
Lakini nikapata muda pia kudurusu maandiko mawili ya kihistoria muhimu kwa Zanzibar. Moja ni lile liloandikwa na Anne Bang linaloeleza historia ya Zanzibar kama kitovu cha elimu, taaluma na wanataaluma wa zama za miaka ya 1900 na ushei. Andiko hili la MEETING PLACE ZANZIBAR, linaeleza jinsi mwanazuoni maarufu mwenye mizizi ya kihadhrami Bwana Ahmad Ibn Sumayt alivyojenga mtandao hadi kwa wanazuoni wa Uturuki akina Bwana Fadhil Pasha na wengine waliohama Hadhramaut kuja Zanzibar na kuifanya Zanzibar kuvuma kwa utukufu wa Elimu.
 
Back
Top Bottom