Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mi siwali hawa ila nilishiriki zoezi la kuwaokota maana wanafamilia huwabugia, zamani walionekana nyakati za mvua za vuli na mwanzo wa mvua za masika, lakini sasa siwaoni misimu hiyo
Wa kwenye vichuguu wengine na hawaliwi. Hawa na senene wana msimu wao. Wanakuja wengi jioni wanaruka wakati wa manyunyu halafu usiku huo wanajikata mabawa yao na kujificha chini ya mawe, majani au kujichimbia chini. Wakijichimbia chini wanaacha alama juu. Kesho yake asubuhi mnajidamka mnaanza kuwafukua huko chini mnawabinya vichwa na kuwatia kwenye vikapu au chombo cho chote. Wakikaangwa na kukaushwa vizuri wanakuwa crunchy basi ni mwendo wa kulala pole pole tu kama walivyo senene.
 
Mwanaume mlo ili upige show za maana.
Siyo kipapatio cha kuku chips tatu
FB_IMG_1563212061142.jpeg
 
Nadhani wanapatikana sehemu kubwa ya nchi, zamani tukiwa wadogo tuliwaokota mitaa ya kwetu TMK, lakini siku hizi siwaoni
Nakumbuka enzi hizo walipatikana sana maeneo ya Chuo cha bandari(Tmk),Tandika maghorofani,Karakana(Tzr) na Yombo mashambani, tulikuwa tunang'ang'aniana na nyoka, mijusi, vyura... Utoto raha sana
 
Back
Top Bottom