Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

.
IMG-20190717-WA0024.jpeg
 
Mwajiriwa hufuata mpango lakini mjasiriamali hutengeneza mpango

Kwa kawaida mwajiriwa hufuata mapango uliowekwa na mwajiri katika utendaji wake wa kazi. Mjasiriamali huweka mipango na kuwa sehemu ya kutekeleza mipango hiyo.

Mwajiriwa hupangiwa kazi lakini mjasiriamali hujipangia kazi yeye mwenyewe.
 
Mwajiriwa huogopa makosa lakini mjasiriamali hujifunza kutokana na makosa

Mwajiriwa huogopa makosa kwani anafahamu makosa hayo yanaweza kumsababishia kupoteza kazi yake. Makosa kwa mjasiriamali ni shule muhimu ambayo itamwezesha kuboresha kile anachokifanya.

Maisha ya ujasiriamali ni kujaribu vitu vingi na kuchagua kile kinacholeta matokeo mazuri.
 
Mwajiriwa hujikita kwenye kitu kimoja lakini mjasiriamali hujaribu vitu vingi

Mwajiriwa hujikita kwenye kazi au nafasi aliyopewa pekee. Mwajiriwa hana haja ya kujaribu vitu vingi kwani yeye hufanya kile alichopangiwa kufanya.

Hali ni tofauti kwa mjasiriamali kwani yeye hufanya vitu vingi kwa njia ya majaribio ili aone kile kinachofanya vizuri zaidi. Kwa njia hii huweza kuchagua kitu chenye tija zaidi.

Mjasiriamali anaweza kuuza chakula leo, kesho nguo, keshokutwa dawa, n.k. ili tu kubaini kile kinachofanya vizuri zaidi.
 
Mwajiriwa hulipwa kutokana na nafasi yake lakini mjasiriamali hulipwa kutokana na matokeo

Nafasi aliyonayo mwajiriwa ndiyo huamua kiwango cha malipo atakacholipwa. Mwajiriwa akiwa mkurugenzi basi atalipwa kama mkurugenzi; lakini mjasiriamali hulipwa au hupata pesa kutokana na matokeo ya kile anachokifanya.

Ikiwa mradi au biashara ya mjasiriamali haitazalisha faida, basi mjasiriamali husika naye hatapata pesa.
 
Mwajiriwa hutafuta muda sahihi lakini mjasiriamali hatafuti muda sahihi

Mara nyingi hakuna muda sahihi wa mjasiriamali. Mjasiriamali huangalia soko na kuanza kujaribu au kufanyia kazi wazo lake.

Hali ni tofauti kwa mwajiriwa, kwani yeye hutafuta muda sahihi wakufanya maamuzi na matendo mbalimbali katika taasisi au ofisi aliyoajiriwa ili kulinda ajira yake.
 
Mwajiriwa huchukua hatari chache lakini mjasiriamali anaishi nazo

Kwa hakika ujasiriamali ni swala lenye hatari au changamoto nyingi, kukubali kuwa mjasiriamali ni lazima uwe umekubali kukabili changamoto na hatari mbalimbali.

Unaweza kuzalisha bidhaa zikakosa soko au ukakabiliwa na changamoto nyingine kama vile kukosa mtaji au mzunguko mdogo wa pesa.

Mwajiriwa hana haja ya kujali sana juu ya hatari kadhaa, kwani kuna watu tayari wapo kwa ajili ya kufanya maamuzi mbalimbali ya taasisi au kampuni iliyomwajiri.
 
Mwajiriwa anafuata ratiba iliyowekwa lakini mjasiriamali anajiwekea ratiba yeye wenyewe

Kauli kama vile “Muda wa kazi umefika” “Muda wa kazi umekwisha” ni kauli unazoweza kuzisikia tu kwa waajiriwa. Mjasiriamali hana muda wa kazi, anatakiwa kufanya kazi kwa bidii kila wakati na kila mahali hadi pale atakapopata matokeo chanya.
 
Back
Top Bottom