Mwajiriwa hujikita kwenye kitu kimoja lakini mjasiriamali hujaribu vitu vingi
Mwajiriwa hujikita kwenye kazi au nafasi aliyopewa pekee. Mwajiriwa hana haja ya kujaribu vitu vingi kwani yeye hufanya kile alichopangiwa kufanya.
Hali ni tofauti kwa mjasiriamali kwani yeye hufanya vitu vingi kwa njia ya majaribio ili aone kile kinachofanya vizuri zaidi. Kwa njia hii huweza kuchagua kitu chenye tija zaidi.
Mjasiriamali anaweza kuuza chakula leo, kesho nguo, keshokutwa dawa, n.k. ili tu kubaini kile kinachofanya vizuri zaidi.