Mshambuliaji wa Real Madrid Gareth Bale anakaribia kuondoka katika klabu hiyo kulingana na mkufunzi wa klabu hiyo Zinedine Zidane.
Mchezaji huyo wa taifa la Wales aliwachwa nje wakati Real Madrid ilipolazwa 3-1 na Bayern Munich nchini Marekani.
Akizungumza baada ya mechi hiyo, Zidane alisema: Tunatumai ataondoka karibuni. Itakuwa vyema kwa kila mmoja wetu.
Tunaandaa uhamisho wake kwa timu nyengine. Sina ubinfasi wowote dhidi yake , lakini inafikia wakati ambao lazima mambo yafanyike.
Bale ambaye ana miaka mitatu iliosalia katika kandarasi yake ameshinda kombe la mabingwa Ulaya mara nne tangu uhamisho wake wa Β£85m kujiunga na Madrid kutokaTottenham mwaka 2013 - ambapo ulivunja rekodi ya dunia mwaka huo.
Akijibu matamshi ya Zidane ajenti wa Bale Jonathan Barnetta aliambia AFP: Zidane ni aibu hana heshima kwa mchezaji ambaye ameifanyia makubwa Real Madrid.
Majeraha yamerudisha nyuma harakati za mchezaji huyo wa Wales akiichezea Real Madrid mara 79 pekee katika misimu minne.
Alicheza mechi 42 msimu uliopita nusu ya mechi hizo akiwa mchezaji wa ziada.