Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir amepiga marufuku wimbo wa taifa kuimbwa katika hafla ambazo hayupo kwa maelezo kuwa wimbo huo ni maalum kwa ajili ya Rais . Kiir amesema wenye ruhusa ya kuimba wimbo wa taifa akiwa hayupo ni Balozi za nchi hiyo na shule pekee. _ Waziri wa Mawasiliano nchini humo Michael Makuei ametangaza kuwa baraza la mawaziri limebariki maamuzi hayo ya marufuku. "Kwa taarifa yenu, wimbo wa taifa ni mahsusi kwaajili ya Rais ahudhuriapo dhifa yoyote na si kuimba wimbo huo na mtu yeyote." Alifafanua.