Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Karani tamba ni miongoni mwa ndege ambao wanapatikana kwa wingi hapa nchini Tanzania hasa huonekana kiurahgisi katika maeneo tengefu ya hifadhi za wanyamapori. Ndege huyu mwenye umbo kubwa ambae ni mla nyama kama jamii ya ndege kipanga na mwewe anapatikana barani Afrika tu. Kutokana na uzuri wa ndege huyu imepelekea baadhi ya mataifa barani Afrika kumuweka ndege huyu katika nembo zao za taifa na mataifa hayo ni Sudani na Afrika ya Kusini. Hii inadhihirisha ni kwa jinsi gani tunapaswa kumtunza ndege huyu hususani hapa nchini kwetu Tanzania ambapo bado tunajivunia uwepo wa ndege huyu katika maeneo mbali mbali.
 
Ndege huyu ameitwa karani kutokana na manyoya yaliyo simama sehemu ya nyuma ya kichwa chake mfano wa karani ya karne ya 18 na alama ya kalamu katika kona ya mbawa zake na hatimae jina karani likatokea kwa ndege huyu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…