Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Ndege hawa wanapendelea sana kutembea kuliko kuruka na wanakadiriwa kuwa na uwezo wa kutembea kilometa 20-30 kwa siku. Japo hupendelea kutembea ila ni warukaji wazuri sana na wana uwezo wa kuruka kimo kirefu sana kwenda angani na wanapo ruka miguu yao mirefu huonekana kuzidi sehemu ya mwili na kuchomoza upande wa nyuma.
 
Karani tamba ni ndege ambae anaishi kwa kujitenga lakini kuna wakati huonekana katika kundi au familia na wanaweza kufikia hadi wa tano. Ndege hawa pia kuishi kwa mipaka na himaya ambapo karani tamba mmoja anaweza kuwa na himaya yenye ukubwa wa kilometa za mraba 50.
 
Karini tamba ni miongoni mwa ndege walao nyama na hupendelea sana kula nyoka, mijusi, vyura, wanyama jamii ya panya, ndege wadogo na mayai ya ndege wengine. Muda mzuri wa mawindo kwa ndege hawa huwa ni mchana kwani wana uwezo wa kuona mchana zaidi kuliko usiku. Japo wakati mwingine hula mizoga ya wanyama ambao wameuwawa katika mazingira yao.
 
Karani tamba huishi wawili katika maisha yao, hii ina maana kwamba dume mmoja huishi na jike wake mpaka nwisho wa maisha yao. Dume hawezi kuwa na jike zaidi ya mmoja hali kadhalika jike hawezi kuwa na dume zaidi ya mmoja. Kabla ya kupandana kwa pamoja dume na jike huwa wanacheza ili kuvutiana na wakati mwingine michezo ya kukimbizana ardhini yote hii ni kumfanya kila mmoja kuwa tayari kwa tendo la kupandana ili waweze kuendeleza kizazi chao kupitia kuzaliana.
 
Hujenga viota kwenye miti jamii ya michingoma, viota hivi hupendelea kujenga kwenye miti yenye urefu wa wastani wa mita 5-7. Kwa pamoja dume na jike hutembelea eneo la kiota kwa muda usiozidi nusu mwaka kabla ya jike kuanza kutaga mayai. Kiota huwa na upana wa takribani mita 2.5 na kimo cha futi moja kwenda chini huku kikiwa na vijiti ambavyo ni bapa sehemu ya chini.
 
Jike hutaga kuamzia yai 1 – 3 na kila yai moja hutagwa kwa tofauti ya siklu 2- 3. Mayai hutamiwa kwa muda wa siku 42-50 na jukumu la kutamia huwa wana shirikiana wote dume na jike japo jike ndio hutumia muda mwingi kutamia mayai kuliko dume. Katika kipindi chote cha kutamia mayai kazi ya kutafuta chakula huwa ni ya dume. Hivyo dume hulazimika kutafuta chakula na kumletea jike katika kiota.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…