Walter alitoa dola 50,000 za kimarekani kwa ajili ya kupata kibali cha kuwinda na akaishia kumuwinda simba ambaye anapendwa na watu wengi, jambo alilolifanya lilimdhalilisha sana, magazeti mengi ya Ulaya na Marekani yaliandika habari za kuuwawa kwa Cecili na mwindaji katili kabisa, mitandao ya kijamii ilimshambulia sana Walter, alipelekwa mahakamani, alifikia hatua akahama hadi nyumba aliokuwa anaishi huko Menesota nchini Marekani na kwenda kujificha hadi hali ilipotulia kidogo mwaka 2016. Hata hivyo kitabu tunachokichambua leo ni matokeo ya gumzo lililotokea duniani baada ya kifo cha Cecil. Silaha aliyoitumia ya upinde na mshale kumuua Cecil ilikuwa njia ya mateso sana, wasaidizi waliokuwa pamoja na Walter wanasema kuwa Cecil alipigwa mshale na kukimbilia porini kujificha na hakufa, kitendo hicho kilisababisha Cecil kupoteza damu nyingi sana kwa muda wa zaidi ya masaa 13, hiyo watu waliona ukatili huo alioufanya Walter wa kumuua Cecil.