Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Jambo la kuuwawa kwa Cecil linatupa kufahamu kwa kina kuwa watu wanapenda sana wanyamapori haswa simba, wanapenda kuwaona wakiwa hai, hata makampuni makubwa ya utalii na uwindaji wanakubaliana na hilo. Hapo ndipo tunapotakiwa kushirikiana katika uhifadhi wa wanyama hawa, sio jambo la nchi moja ni dunia nzima.
 
Picha ambayo ipo kichwani kwangu ni hii, wawindaji hawa amabao wanakuja kwenye hifadhi zetu na kutoa vihela kidogo wanaua wanyama wetu wa thamani ili kwenda kuweka kama mapambo katika majumba yao ya kifahari wanapewa heshima kubwa sana katika nchi zetu za Afrika. Hakuna vitu vya maana sana ambavyo vinaweza kuhalalisha uwindaji kuwa jambo muhimu sana endapo hatutabadili jinsi tunavyozichukulia rasilimali zetu.
 
Jambo la kuuwawa kwa Cecil linatupa kufahamu kwa kina kuwa watu wanapenda sana wanyamapori haswa simba, wanapenda kuwaona wakiwa hai, hata makampuni makubwa ya utalii na uwindaji wanakubaliana na hilo. Hapo ndipo tunapotakiwa kushirikiana katika uhifadhi wa wanyama hawa, sio jambo la nchi moja ni dunia nzima.
 
Picha ambayo ipo kichwani kwangu ni hii, wawindaji hawa amabao wanakuja kwenye hifadhi zetu na kutoa vihela kidogo wanaua wanyama wetu wa thamani ili kwenda kuweka kama mapambo katika majumba yao ya kifahari wanapewa heshima kubwa sana katika nchi zetu za Afrika. Hakuna vitu vya maana sana ambavyo vinaweza kuhalalisha uwindaji kuwa jambo muhimu sana endapo hatutabadili jinsi tunavyozichukulia rasilimali zetu.
 
Kwa upande mwingine mwananchi masikini ambaya anaishi kando ya hifadhi za wanyama hawa anapoingia porini ili kujipatia mnyama mdogo kwa ajili ya chakula na virutubisho vingine muhimu kama protini anapokamatwa anaishia kupigwa vibaya, kufungwa jela na hata kuwawa. Ikumbukwe mtu huyu anatafuta wanyamapori kwa ajili ya mahitaji muhimu kama chakula nk. Lakini mara nyingi akikamatwa anachukuliwa kama jambazi au jangili hivyo maisha yake yanakuwa hatarini.
 
Kwa kusema hivyo sio kwamba nahalalisha jamii kuingia porini na kuwinda wanyama kama chakula, la hasha, tunatakiwa tubadili mitazamo yetu na sera zetu ili mwananchi ambaye ndiye mhanga wa wanyama hawa aone faida kubwa ya uwepo wa wanyamapori hawa kuliko kuingia porini na kuanza kuwinda. Tunawapa heshima wawindaji wakubwa na makampuni yao kwa kuwa ni watu matajiri na wanaotoa fedha; lakini wengi hawajui chochote kuhusu gharama ambazo watu na nchi yetu inaingia katika uhifadhi wa wanyamapori.
 
Nimejifunza jamii zetu hasa zinazoishi kando ya hifadhi za wanyamapori ni wavumilivu sana na wamekuwa wakivumilia hasara kubwa sana zinazoletwa na wanyamapori walio karibu yao. Kama ni wakulima wanapata hasara kwa tembo au wanyama wengeni wanaokula majani kuharibu mazao na mashamba yao, kama ni wafugaji wanapata hasara kwa simba na wanyama wengine kama fisi, duma na chui kula mifugo yao. Kwa haraka mzunguko mzima na mtazamo walionao ni hasara kubwa kuliko faida. Tunatakiwa kubadili sera na sheria zetu kwenye eneo hili la uwindaji na uhifadhi kwa ujumla ili manufaa makubwa yabaki kwa wananchi waishio maeneo yaliyo karbu na wanyamapori.
 
Licha ya hayo, kuna changamoto nyingine nyingi wanazokutana nazo simba wawapo porini hasa kwenye maeneo yao, utafiti wa Andrew ulionyesha namna simba wengi walivyokamatwa na mitego ya majangili iliyotegwa kwa lengo la kuwakamata wanyama wengine. Mitego hii ipo maeneo mengi sana kwenye maeneo ya wanyamapori na inawakamatwa hata wanyama ambao hawajakusudiwa, kwa kweli simba wengi wanaokamatwa katika mitego hiyo sio rahisi kupona na kuendelea na maisha yao.
 
Mara nyingi sana kwa nchi masikini ambazo zina wanyamapori ni nadra sana kuona uhifadhi ikiwa katika ajenda kuu za nchi. Nchi nyingi masikini hazina mahitaji muhimu kwa ajili ya kusaidia maisha ya wananchi wake yawe bora. Hivyo kutakuwa na ajenda nyingi sana za kuleta na kuharakisha maendeleo, ambazo ndizo hutengewa fedha nyingi za kuendesha sekta hizo, mfano ni sekta ya afya, elimu, kilimo na sekta ya miundombinu.
 
Kwa changamoto za kiuchumi ambazo zinawagusa wananchi wengi imekuwa ndio msingi wa siasa za viongozi wengi wa nchi masikini, watatumia changamoto hizo kama mtaji wa kupata uongozi na nafasi nyingine za juu kwenye serikali. Hivyo hata wakati wa kupitisha na kuandaa bajeti za maendeleo ni bajeti kiasi kidogo sana zinazoelekezwa kwenye kukuza uhifadhi na mazingira asilia ya wanyamapori.
 
Hata hivyo, nchi nyingi masikini hupata misaada kuoka nchi tajiri ambazo watu wake wana vyanzo vingi na vya uhakika vya kipato hivyo hutoa kodi kubwa na kutosheleza mambo yote muhimu kwa wananchi wake, tofauti na nchi masikini ambazo zikipata misaada hiyo hugawanywa sana na kufanya isitoshe hata katika uwekezaji wa sekta mbazo ni muhimu zaidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…