Kwasababu ya udhaifu huo, maliasili zetu muhimu zimekuwa zikipeperushwa na ndege, meli, magari na bandari zetu, viwanja vyetu vya ndege na barabara zetu zimekuwa njia za zikisafirishia maliasili zetu muhimu kwenda kwa matajiri wakubwa kwenye nchi za nje. Hii ndio sababu katika nchi masikini ujangili wa wanyamapori umekithiri sana. Hadi nchi hizi masikini zije kuwa sawa na kuamua sasa zinawekeza vya kutosha katika sekta hii, inaweza isitokee au inaweza kuja kuwa tumeshachelewa sana.