Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kwa sasa jezi hiyo inasemekana ni kama vile ina mikosi. Washambuliaji wengi wanaovaa jezi hiyo pale Chelsea katika miaka ya karibuni wamefeli. Alvaro Morata, Fernando Torres, Radamel Falcao, ni miongoni mwa mastaa ambao wamefeli katika jezi hiyo.

Kuna laana au mikosi mingi ambayo imekuwa ikihusishwa na soka.
 
Mwanamuziki maarufu wa kike duniani, Whitney Houston alifariki mwaka 2012 saa chache baada ya Ramsey kuisaidia Arsenal kuichapa Southampton. Lakini pia Mwigizaji maarufu, Alan Rickman alifariki siku moja baada ya staa huyu wa Wales kuiwezesha Arsenal kuichapa Liverpool.
 
Abraham aliyekulia katika kikosi cha vijana cha Chelsea ana kazi ngumu ya kuondoa mkosi katika jezi namba 9 ya Chelsea. Sio jezi nzuri kuikimbilia ukizingatia washambuliaji mahiri wanakwenda pale na sifa lukuki lakini wanashindwa kuonyesha makali yao wakivaa jezi hii. Gonzalo Higuain licha ya makali yake lakini alifunga mabao matano tu na jezi hii kuanzia Januari mwaka huu.
 
Kabla ya hapo mastaa wakubwa kama Alvaro Morata, Fernando Torres, Radamel Falcao na Mateja Kezman wote walivaa jezi hii lakini bila ya mafanikio yoyote. Abraham amezungumzia kuhusu mkosi huo kwa majigambo makubwa huku akisema: “Nimesikia upuuzi kuhusu jezi namba 9. Niko hapa kucheza soka langu na kujaribu kila ninachoweza.
 
Mkosi wa kupiga picha na Drake

Mamilioni ya mashabiki wa muziki duniani kote wanatamani kupiga picha na rapa maarufu wa Canada, Drake.

Hata hivyo, kwa sasa watu wameanza kujifikiria mara mbili kupiga picha na Drake. Imeibuka tabia ambapo kila unapopiga picha na rapa huyu unaelekea kushindwa katika mchezo unaoshiriki. Mastaa wengi wa soka wamejikuta wakichemsha katika hili na mmojawapo ni kiungo wa Manchester United ambaye alipiga picha na Pogba saa chache kabla ya Manchester United haijachapwa na Wolves 2-1 Kombe la FA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…