Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Vipande vipande vilivyovunjika kutokana na mkwaruzano wa dunia na Kitu hicho ( MARS EVIL TWIN) vilitupwa na vikajikusanya pamoja umbali wa kilometa 384,400 kutoka katika sayari yetu ya dunia ndipo vikatengeneza Mwezi. Kitendo hiki kilifanyika katika muda kama wa mwaka mmoja tu.
 
JE KUNA MIEZI MINGINE AMBAYO HATUIONI?
Sayari ya Dunia ina mwezi mmoja tu. Mwezi wa Dunia una jina lake ambalo ni LUNA. Watu wengi wamezoea kuiita mwezi wa dunia kama "MOON" kwa sababu hapo mwanzoni haikufahamika kama kuna miezi mingine mingi (other moons) zaidi ya huu wa dunia mpaka pale mwanasayansi wa Elimu ya anga GALILEO GALILEI alipogundua miezi mingine mnne (4) ya sayari ya Jupiter hii ilikua mwaka 1610.
 
Karibu kila sayari imezungukwa na miezi yake. Tunaweza kuuona mwezi wa dunia kwa sababu ndio mwezi wake, Dunia ina mwezi mmoja tu ambao tumesema unaitwa LUNA.
Sayari nyingine pia zina miezi yake, mfano sayari ya SATURN imezungukwa na miezi yake 53 baadhi ya majina ya miezi hiyo ya saturn ni MIMAS, PANDORA, TITAN, DIONE, TETHYS, ENCELADUS, RHEA, HYPERION, EPIMETHEUS, PROMETHEUS, PAN, na mengine mengi.
 
Wakati sayari ya JUPITER nayo ina miezi yake 53 inayoizunguka, na Jupiter ndio sayari yenye mwezi mkubwa zaidi kupita miezi yote inayopatikana katika sayari nyingine. Mwezi huo mkubwa wa Jupiter unafahamika kwa jina la GANYMEDE, wanasayansi wanasema mwezi huu ni mkubwa kiasi kwamba unaweza tu kuuona kwa kutumia darubini ya kawaida.
 
Miezi mingine ya Jupiter ni EUROPA, IO (tamka Ayi -oh) na CALLISTO.
Idadi ya miezi inayopatikana katika sayari nyingine ni kama ifuatavyo; Sayari ya URANUS ina miezi 27, Sayari ya NEPTUNE ina miezi 13 wakati sayari ya MARS yenyewe ina miezi 2 tu. Ambayo ni Phobos and Deimos.
 
JE MWEZI HUWA UNAWAKA NDIO MAANA TUNAUONA MWANGA USIKU?
Mwezi hauna muanga wake. Mwezi ni miamba na vumbi tu. Udongo wa Mwezi upo katika namna ambayo unauwezesha KUAKISI mwanga mwingi zaidi (the moon reflects the sunlight that hits, it reflects more light back towards the Sun than in other directions) unaomulika kutoka kwenye JUA na kuurudisha katika uelekeo wa jua zaidi kuliko uelekeo mwingine.
 
Mwezi kuonekana umewaka sana au upo nusu inategemeana upo upande gani katika muhimili wake. Ndio mwezi pia unazunguka katika muhimili wake(orbit) huku ukiizunguka dunia.
Wakati huu mwezi unaizunguuka dunia kuna wakati sehemu yote inayomulikwa na jua tunaiona hapa usiku - hii ndio kitaalamu huitwa FULL MOOM au mwezi mzima.
 
Lakini kadri mwezi unavyoizunguuka dunia kuna wakati si sehemu yote ya mwezi inayomulikwa na jua inaonekana upande wetu wa dunia, kuna wakati tunauona Mwezi kama kipande cha kucha iliyokatwa baada ya kuwa upande wa mwezi unaomulikwa hatuuoni, hapa tunaita MWEZI MCHANGA (NEW MOON) na ndivyo unavyobadilika kutoka mwezi mchanga, nusu na mzima.
 
Tunauona mwezi kwa macho kwa sababu umbo lake ni kubwa, lakini ukweli ni kwamba mwezi upo mbali sana na dunia yetu tofauti na tunavyofikiri. Umbali wa kutoka sayari ya dunia mpaka mwezini ni kilometa Laki Tatu Themanini na Nne Elfu na Mia Nne (384,400 kilometers).
 
JE KUNA UHUSIANO GANI WA MWEZI NA DUNIA
Wanasayansi wamekubaliana katika hoja kua mwezi ndio unaruhusu maisha ya viumbe hai yaendelee katika Sayari ya Dunia. Hoja hii imeegemea katika mambo yafutayo ambayo Mwezi unaifanyia dunia
 
Mwezi huvivuta vitu vingi sana vikubwa angani ambavyo huwa vinaelekea kuigonga dunia na ambavyo kama mwezi usingevivuta na vikaangukia katika uso wa dunia basi vingeleta madhara makubwa sana hapa duniani ikiwa ni pamoja na kuua viumbe wote.
Uthibitisho wake ni mabonde makubwa na mashimo yanayopatikana mwezini amabyo yanadhibitisha kwamba yalitokea baada vya vitu vyenye uzito mkubwa kuvuta na kuangukia hapo.(Our moon is basically great attractor of all things that want to hit the Earth).
 
Kupwa na Kujaa kwa Bahari (Ocean Tides) or ( Lunar Tides)
Kupwa na kujaa kwa maji hutokea baharini na pia kwenye maziwa makubwa, mwezi na dunia siku zote huvutana, mwezi huwa unajaribu kuvuta chochote kilichopo duniani ili ikisogeze karibu wakati huo huo dunia nayo huvivuta vitu vyake viendelee kubaki katika dunia. (The Earth’s gravity against The moon's Gravity)
Maji ni kitu kisichotulia sehemu moja na hubadirika umbo kirahisi sana, hivyo mvutano huu huyafanya maji kuelekea kule mwezi ulipo na hapa ndio kitendo cha kupwa na kujaa kwa maji pamoja na mawimbi kutokea baharini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…