BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,767
- 288,340
Umeenda deep sana mkuu [emoji16][emoji16][emoji16]
π΄π΄
Mimi nina miaka 37, nilikua naishi na mwanamke ambaye hatujafunga naye ndoa na tuna watoto wawili, mara kadhaa tumekua tunagombana, namuambia tuachane anaomba msamaha tunarudiana. Mara nyingio tunagombana naye kwakua ana mdomo sana, ni mtu wa kulalamika hasa suala la ndoa kwani tumekaa pamoja miaka 10 bila ndoa kama mke na mume. Mimi nimekua nikimuambia subiri subiri tunagombana namrudisha kwao anaomba msamaha anarudi. Sababu ya kuja kwako nikuwa, mwezi uliopita tuligombana sana, kuna meseji aliziona kwenye simu yangu, zilikua za mapenzi kweli nakiri nilikosea lakini kama mwanaume sikujishusha, nilimpiga akatishia kuondoka nikamuambia aondoke. Nilijua hataondoka lakini nilipomuona yuko siriasi nilimuambia kama anataka kuondona basi aondoke lakini aniachie wanangu. Alirudi ndani nikaenda kazini, nikijua kuwa yameisha nilirudi kaondoka naacha watoto wadogo na binti wa kazi. Nilimpigia simu hapokei, nikajua kaenda kwao, nilikaa siku tatu nikijua kuwa lazima atarudi lakini nilipompigia simu Mama yake kumsalimia alionekana kama hajui chochote. Nililazimika kumuuliza akasema mke wangu hajarudi kwake na wala hajui kama tuna ugomvi, nilipata wasiwasi kidogo, nikaanza kutafuta rafiki zake nikijua kuwa yuko huko. Walinizungusha kuniambia lakini wakisema kuwa yuko salama. Lakini sikuridhika nilienda Polisi ili kikitokea kitu niwe salama. Nimekaa karibu mwezi mke angu ananipigia simu kuwa you Geita kuna mwanaume kampata na wameshafunga ndoa hivyo yeye ni mke wa mtu nisimtafute. Nilipigia ndugu zake wakaniambia nikweli mdogo wake wakiume ndiyo aliruhusu aolewe na wamefunga ndoa ya kiislamu kwani mimi nilikataa kumuoa. Nimechanganyikiwa kwakweli, namuambia kuhusu watoto kuwa siwezi kumruhusu awaone anaonekana kama hajali. Ananijibu kwa dharau kuwa hao ni wanao lea tu nitakuja kusalimia. Yaani mke wangu hajali kabisa na sijui nifanye nini? Naomba ushauri hata kisheria iko vi[pi, je ndoa hiyo inatambulika kwakua mimi nilishaishi muda mrefu kama mke na mume je si nilitakiwa kumpa talaka kwanza? Mimi bado nampenda na najua ni hasira tu ambazo zimemfanya kuchukua maamuzi ya haraka akisahau kuwa tumetoka mbali, je naweza kumshitaki nikarudiana nae?...Naomba ushauri wako
Naomba ushauri wako kwani nimechanganyikiwa na sijui kama nifanye nini? Mimi ni kijana wa miaka 37, sijaoa ila nilikua naishi na mwanamke kwa miaka 8 bila ndoa. Kila wakati alikua ananiambia kuhusu ndoa lakini niliogopa kufunga naye ndoa kwakua nina mali zangu nilijua kuwa kama nikifunga naye ndoa ikitokea tukaachana basi tutagawana mali. Yeye alikua anafanya kazi lakini nilimuambia kuwa aache kazi akawa anasimamia biashara zangu, kweli ana akili ya biashara hata kuliko mimi. Mungu ametujaalia watoto wawili, kuna mambo mengi ambayo tumekua tukikorofishana lakini kubwa alikua analalamika kuhusu ndoa. Alipolalamika sana nilienda kujitambulisha kwao nikatoa kishika uchumba basi kweli sikurudi tena. Sasa sababu ya kuja kwako niligundua kuwa huyu mwanamke ni mshenzi, kwamba pamoja na kumbana sana katika baishara lakini kuna namna alikua anaiba na nilipofuatilia nikagundua kuwa kajenga nyumba zake mbili na ana biashara huko kwao ambayo mdogo wake anasimamia. Nilikasirika na kweli nilimpiga, hapo nilikosea, aliondoka kwenda kwao akaondoka na wanangu. Lakini ndugu zangu waliingilia kati tukaenda kuchukua watoto wetu. Watoto nipo nao hapa wapo na Dada yangu, sasa nilipoona amekaa muda mrefu hataki kurudi nilichukua mwanamke mwingine na kuanza kuishi naye. Sikua nampenda kwani kikubwa nikuwa mke wangu alikua na nyota ya biashara, nilifanya hivyo ili kumuumiza mke wangu aje kuniomba msamaha. Nimekaa na huyu mwanamke mwezi wa sita sasa mke wangu haji kuniomba msamaha. Nimechunguza hana mwanaume mwingine, sababu ya kuja kwako ni hivi, mimi kuna mikopo nilichukua benki kwaajili ya biashara ila hali ya biashara baada ya yeye kuondoka imekua ngumu sana. Kule kwao ana nyumba mbili kajenga na pesa yangu na biahsara yake inaenda vizuri je kuna namna yoyote ya kumlazimisha yeye kulipa deni pamoja na mimi. Kwa maana tumekaa kama mke na mume na najua hivyo vitu vyake kachumia kwangu kwanini mimi vitu viuze wakati wote tumefaidika. Kibaya nikuwa anatamba hawezi kurudi kwangu ana furaha na mimi sitaki arudi ila nataka kujua kisheria si deni unalipa wote? Endelea kufuatilia @iddmakengo
Muandiko kama wa mtu mmoja..... ni kweli au story tuu?ushauri wako, mimi ni kijana nina miaka 28, sijaoa ila nina mchumba ambaye tuko kwenye mahusiano kwa miaka mitano sasa na ana ujauzito wangu wa miezi nane. Nasema bado nimchumba wangu kwani sijamuacha rasmi ingawa nimeoa mwanamke mwingine. Labda nifafanue kidogo sio kwamba mimi ni Malatya hapana, baada ya huyu mchumba wangu kupata ujauzito nilienda kujitambulisha kwao, nilipanga kumuoa na kweli walinikubali, lakini shida ilikua ni kwetu, baada ya kumtambulisha wazazi wangu walimkataa. Walitoa kisingizio cha kabila na kusema kuwa yule mwanamke kwao wana uwezo mkubwa wa kifedha hivyo atanisumbua. Mimi nilikua nampenda lakini nguvu ya wazi ilikua kubwa hivyo walinilazimisha kumuoa mwanamke mwingine ambaye tulifunga naye ndoa kijijini. Nilifanya kimya kwani sikutaka kumuudhi mchumba wangu, nilitaka kusubiri mpaka ajifungue ndiyo nimuambie ili ikiwezekana nimuoe mke wa pili. Lakini Dada yangu alimpigia simu, akamtumia mpaka picha za harusi na kumuambia kuwa anapoteza muda. Aliniuliza nikamuambia nikweli lakini sikuoa kwa mapenzi yangu bali kwa kulazimishwa, alikasirika akisema ndoa hailazimishwi, aliniambia tusijuane kaniblock. Wakati huo alikua na ujauzito wa miezi mitatu, nilijua tu kuwa kwakua ana mimba hawezi kwenda popote atarudi akijifungua. Nilikaa kimya kwa miezi mtano hivi ndipo nikapata tetesi kuwa yupo karibu na Kaka mmoja ambaye ni mfanyakazi mwenzake, huyu Kaka alikua anamsumbua sana tangu zamani anamtongoza lakini mchumba wangu alimkatalia. Sasa ninachoona ni kwamba katumia fursa ya huu upweke na anamdanganya, nilipogundua nikamtafuta nikaongea naye akaniambia kuwa ni kweli yuko na huyo Kaka kwani amekua karibu naye muda mrefu kipindi mimi sipo hivyo ameamua kumpa nafasi atajifunza kumpenda kwakua mimi nishaoa na huyo mwanaume yupo tayari kumlea mwanangu. Nimeumia sana kwani nampenda sana mchumba wangu lakini yeye ameshindwa kuwa mvumilivu, sisi ni waislamu ningeweza hata kumuoa mke wapili lakini hataki, nimemuambia anipe muda hata nigombane na mke wangu tukiachana ndiyo nimuoe hataki, yaani hapa nimechanganyikiwa, kila nikifikiria mchumba wangu yupo na mtu mwingine naumia najikuta na hasra hata m
Stupid man [emoji36][emoji36][emoji36]Mimi nina miaka 37, nilikua naishi na mwanamke ambaye hatujafunga naye ndoa na tuna watoto wawili, mara kadhaa tumekua tunagombana, namuambia tuachane anaomba msamaha tunarudiana. Mara nyingio tunagombana naye kwakua ana mdomo sana, ni mtu wa kulalamika hasa suala la ndoa kwani tumekaa pamoja miaka 10 bila ndoa kama mke na mume. Mimi nimekua nikimuambia subiri subiri tunagombana namrudisha kwao anaomba msamaha anarudi. Sababu ya kuja kwako nikuwa, mwezi uliopita tuligombana sana, kuna meseji aliziona kwenye simu yangu, zilikua za mapenzi kweli nakiri nilikosea lakini kama mwanaume sikujishusha, nilimpiga akatishia kuondoka nikamuambia aondoke. Nilijua hataondoka lakini nilipomuona yuko siriasi nilimuambia kama anataka kuondona basi aondoke lakini aniachie wanangu. Alirudi ndani nikaenda kazini, nikijua kuwa yameisha nilirudi kaondoka naacha watoto wadogo na binti wa kazi. Nilimpigia simu hapokei, nikajua kaenda kwao, nilikaa siku tatu nikijua kuwa lazima atarudi lakini nilipompigia simu Mama yake kumsalimia alionekana kama hajui chochote. Nililazimika kumuuliza akasema mke wangu hajarudi kwake na wala hajui kama tuna ugomvi, nilipata wasiwasi kidogo, nikaanza kutafuta rafiki zake nikijua kuwa yuko huko. Walinizungusha kuniambia lakini wakisema kuwa yuko salama. Lakini sikuridhika nilienda Polisi ili kikitokea kitu niwe salama. Nimekaa karibu mwezi mke angu ananipigia simu kuwa you Geita kuna mwanaume kampata na wameshafunga ndoa hivyo yeye ni mke wa mtu nisimtafute. Nilipigia ndugu zake wakaniambia nikweli mdogo wake wakiume ndiyo aliruhusu aolewe na wamefunga ndoa ya kiislamu kwani mimi nilikataa kumuoa. Nimechanganyikiwa kwakweli, namuambia kuhusu watoto kuwa siwezi kumruhusu awaone anaonekana kama hajali. Ananijibu kwa dharau kuwa hao ni wanao lea tu nitakuja kusalimia. Yaani mke wangu hajali kabisa na sijui nifanye nini? Naomba ushauri hata kisheria iko vi[pi, je ndoa hiyo inatambulika kwakua mimi nilishaishi muda mrefu kama mke na mume je si nilitakiwa kumpa talaka kwanza? Mimi bado nampenda na najua ni hasira tu ambazo zimemfanya kuchukua maamuzi ya haraka akisahau kuwa tumetoka mbali, je naweza kumshitaki nikarudiana nae?...Naomba ushauri wako
Kanichekesha sanaStupid man [emoji36][emoji36][emoji36]
Nimezikuta kwenye page ya iddmakengo insta. Kama hauna insta google kama mie utaziona na watu wanatoa ushauriMuandiko kama wa mtu mmoja..... ni kweli au story tuu?
Jamaa kapiga fasta fasta mke tulii ananyonyesha now kapili
Lamba Lolo Ni kitu siwezi kufafanua saudi ya vile nilielezea..Kulamba "lolo" ni ndiyo nini mkuu