Manuel Beshara (5) mkazi wa Jimbo Florida, nchini Marekani alipiga namba ya dharura polisi, 911, na kuwaambia kuwa ana njaa, na kwamba alitaka kuagiza pizza. Polisi walikwenda hadi anapoishi, wakamuelezea matumizi sahihi ya namba hiyo, kabla ya kununua pizza na kumpelekea.