Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

IMG-20190814-WA0001.jpeg
 
Liverpool ilicheza mechi ya kwanza Ijumaa na kushinda 4-1 dhidi ya Norwich City, wakati Mabingwa watetezi Manchester City ikishinda 5-0 dhidi West Ham, Arsenal ilipata ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Newcastle United huku Manchester United ikifunga pazi la ufunguzi kwa kuichapa Chelsea kwa mabao 4-0.
 
Chelsea wana wakati mgumu

Inaonekana wazi tayari, Chelsea wameanza ligi vibaya kipigo cha aibu ya 4-0 mikononi mwa Manchester United, huku pengo la nyota wao Eden Hazard likijionyesha wazi katika mchezo huo.
 
Mbali ya ushambuliaji bado safu ya ulinzi ya Chelsea imepata pigo lingine baada ya kuondoka kwa beki David Luiz aliyejiunga na Arsenal, jambo lililochangua kwa sehemu moja kipigo cha mabao 4-0 kutoka kwa Man United.
 
Kwa hali hii kocha wa Chelsea, Frank Lampard atakuwa na wakati mgumu na kikosi hicho maana ukiangalia timu nzima haina mawasiliano wanacheza kama timu nzima ni wageni.
 
Hatimaye Manchester United wamepata mfumo wa kushinda

Wakati Jumapili ilikuwa siku mbaya kwa Chelsea, hali ni tofauti kwa Manchester United. Mashetani wekundu walitekeleza mpango wao wa mchezo kuwa kamili kwa shambulio la nguvu la kuiteketeza The blues.
 
Back
Top Bottom