Porto na Celtic zimeanga mapema mashindano ya Ligi ya mabingwa huku Ajax ikiponea tundu la sindano kufuzu kwa hatua ya mwisho ya kucheza hatua ya makundi ya mashindano hayo,
Mabingwa 2004, Porto wanashinda kufuzu kwa mara ya kwanza kwa hatua ya makundi tangu msimu 2010-11, wakati Celtic ikirudia rekodi yake mbaya ya msimu uliopita.
Mabingwa hao wa Ureno, Porto ilishinda mchezo wa kwanza bao 1-0, lakini katika mchezo wa marudiano walikubali kuruhusu mabao 3-0 kutoka kwa FC Krasnodar ya Russia kwenye Uwanja do Dragao.