Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

ba1dd4bc6ff065668dc667a6a008b6fe.jpeg
 
Mkutano huo ambao awali ulipangwa kufanyika Septemba 11 kwenye makao makuu ya chombo hicho mjini Nyon, kilitarajiwa kukutanisha viongozi wa Chama cha Klabu za Ulaya (ECA), viongozi wa ligi z Ulaya na wawakilishi kutoka sehemu mbalimbali za Ulaya.
 
Lakini katika barua iliyoonwa na AFP ambayo imetumwa kwa rais wa ECA, Andrea Agnelli, kiongozi wa Ligi za Ulaya na Lars-Christer Olsson iliyotumwa na rais wa Uefa Aleksander Ceferin, inasema "ameamua kuahirisha kikao cha Septemba 11".
 
Kwa sasa tuko kwenye mchakato wa kukusanya maoni kutoka vyama vya soka vya nchi na nahisi –- kwa ujumla zaidi –- kwamba mazungumzo mapya sasa yatakuwa yamewahi sana kwa kuwa tunachambua maoni na mapendekezo kutoka pande tofauti," ameandika Ceferin.
 
Kwa mujibu wa taarifa zilizoripotiwa, ligi ya juu ingekuwa na makundi manne ya timu nane na timu sita kutoka katika kila kundi zikifuzu kucheza hatua inayofuata bila ya kujali nafasi ambazo timu hizo zimeshika katika ligi ya nyumbani.
 
Agnelli alitetea mpango huo akisema ni jaribio la kuziokoa klabu ndogo dhidi ya ligi tano kubwa.
Hata hivyo Ligi Kuu ya England, ambayo iliingiza timu nne katika fainali za Ligi ya Mabingwa na Kombe la Europa, imepinga pendekezo hilo kwe akauli moja
 
Juni 15, klabu za Ligi Kuu ya Italia (Serie A) ambako kuna timu ya Agnelli ya Juventus iliyoshikilia ubingwa kwa takriban muongo mmoja, zilipinga pendekezo la mageuzi hayo, huku Juve ikiwa klabu pekee iliyounga mkono.
Klabu zilizopinga za Serie A, ambazo ni pamoja na Napoli na Lazio, zinaamini kuwa kuwa mpango huo unaweza kusababisha kupunguza mapato ya mechi za ligi hiyo kwa hadi asilimia 35.
 
Klabu saba za Hispania, lakini si Real Madrid wala Barcelona, pia zinapinga mpango huo sambamba na klabu za Ujerumani (Bundesliga), wakati timu 17 za Ufaransa pia zimepinga wakati Paris Saint-Germain, Lyon na Marseille hazijaweza misimamo yao.
 
Back
Top Bottom