Maji ya mvua ni rahisi kuvunwa kutoka kwenye paa za nyumba na kukusanywa kwenye vyombo vya kuhifadhia kama vile mapipa au matenki yaliyoweka pembeni ya nyumba.
Paa ambazo zimetengenezwa kutokana na madini chuma yakiwemo risasi, asbesto, au lami yana kemikali zenye sumu ndani yake ambazo huyafanya maji hayo kutokuwa salama kwa ajili ya kunywa
Kuyafanya maji kuwa salama kwa ajili ya kunywa
Kuyafanya maji kuwa salama kwa ajili ya kunywa ni njia bora zaidi mojawapo ya kuzuia kuharisha na magonjwa
Hata kama maji yatakuwa yanaonekana safi kwa macho na kutiririka kutoka bombani, kwenye matenki, au visimani, hii haimaanishi kuwa hayajafuliwa au hayahitaji kutibiwa.
Katika kuamua njia gani ya kutibu maji itumike, fikiria juu ya kiasi cha maji unachohitaji., yamechafuliwa na nini, na rasilimali zilizopo kwa ajili ya kazi ya kuyatibu.