Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kama maji yako yana uchafu, kwanza ruhusu yatulie kwenye chombo kwa saa kadhaa ili uchafu, na vijidudu vya magonjwa viweze kusuka chini ya chombo. Mwaga maji yaliyotulia kwenye chujio. Usijaribu kutikisa uchafu uliotulia chini ya chombo. Halafu safisha chombo.
 
Chujio za kitambaa
Katika nchi za Bangladesh na India, watu hutumia chujio iliyotengenezwa kutokana na kitambaa chenye nyuzi zilizoshonwa vizuri kwa karibu kuondoa vijidudu vya kipindupindu kwenye maji. Vijidudu vya kipindupindu mara nyingi hujibanza kwenye mnyama mdogo yoyote aishiye majini, na zoezi la kuchuja na kuwatoa nje wanyama hao pia huondoa vijidudu vingi vya kipindupindu. Unaweza kutengeneza chujio la kitambaa kutokana na vitambaa vya mkononi, vitambaa vya pamba na vitambaa vingine vyenye nyuzi zilizofungamana vizuri. Nguo zilizowahi kutumika hufanya kazi vizuri kwa sababu nafasi katika nyuzi za nguo zilizotumika huwa zinakuwa zimepungua sana na hivyo kuchuja vizuri.
 
Ruhusu maji yatulie kwenye chombo ili uchafu utue chini.
Kunja kitambaa mara 4,tanua au funga juu mdomo wa chombo kingine au jagi.
Mwaga maji polepole kutoka kwenye chombo cha kwanza kwenda chombo kingine kupitia chujio la kitambaa. Kila mara tumia upande mmoja wa kitambaa, au vijidudu vitaingia kwenye maji.
Baada ya kutumia kitambaa, fua na kukausha juani. Hii huua vijidudu ambavyo vinaweza kuwa vilibaki kwenye kitambaa.Wakati wa msimu wa mvua, tibu kitambaa kwa kutumia dawa maalum ya kuwa vijidudu (bleach)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…