Katika dunia hii ya leo ni vigumu kuishi bila kutumia intaneti kwa namna moja au nyingine. Watu hutumia intaneti kuwasiliana, kupata taarifa na habari au hata kujipatia kipato.
Swala hili limepelekea baadhi ya nchi na mashirika mbalimbali kujaribu kukabili taarifa mbalimbali zinazopatikana kwenye mtandao ili kupunguza athari zinazoweza kusababishwa na taarifa hizo.
Ni vyema kuhakikisha tovuti au blog unayochukua taarifa inaaminika ili usije ukapotoshwa na taarifa za uongo.
Mtu anaweza kuwa Iran akamdukua mtu au tovuti iliyoko Marekani bila kizuizi chochote. Hivyo ni muhimu kuwa makini pamoja na kuzingatia kanuni za usalama kwenye mtandao ili uwe salama mara utumiapo intaneti.
Ni rahisi mtu kuwa mtawaliwa wa mtandao wa intaneti (internet addict). Baadhi ya watu hukaa siku nzima kwenye mtandao wa intaneti au hushindwa kutimiza majukumu yao ya kila siku kwani wao kila mara wako kwenye mtandao.