Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

455930763_440879.jpeg
 
Kama kuna kitu kinamchanganya kwa sasa Pep Guardiola ni VAR. sio kama haipendi, hapana, anadai inachagua matukio. Anaishangaa na anaamini inatumika vibaya,
Juzi Jumamosi, kocha huyo wa Manchester City alishuhudia kwa mara nyingine VAR ikiinyima ushindi timu yake dhidi ya Tottenham baada ya bao la Gabriel Jesus kukataliwa katika dakika za majeruhi.
 
Bao hilo la dakika ya 92 ambalo lingekuwa la ushindi kwa City lilikataliwa kwa madai beki wa City, Aymeric Laporte aliunawa mpira kabla ya Jesus hajafunga. Na sasa Guardiola amedai VAR haikutumikia vema katika maeneo yote.
 
Kocha huyo ametoa mfano wa mpira ulioguswa na mkono na beki wa Chelsea, Andreas Christensen katika pambano la Super Cup dhidi ya Liverpool Jumatano iliyopita lakini mwamuzi hakutoa penalti. Lakini pia akaelezea bao lililokataliwa la Wolves dhidi ya Leicester City ingawa mazingira yalikuwa kama ya Christensen.
 
Kwanini haikupigwa filimbi wakati Llorente aliponawa msimu uliopita lakini leo imepigwa filimbi? Wakati mwingine wanaamini mchezaji amegusa wakati mwingine hawaamini. Ilitokea wiki iliyopita kwa Wolves na tuliona kwa Chelsea Jumatano. Golikipa hakuwa katika mstari (Adrian) wakati penalti inapigwa,” alisema Guardiola.
 
Guardiola pia alilalamika VAR haikuwapa penalti wakati Erik Lamela alipomkaba shingoni kiungo wake, Rodri ndani ya boksi juzi kabla ya mapumziko.
“Ni penalti. Rodri alikwenda chini lakini wakati huo VAR ilikuwa inakunywa kahawa. Inabidi uone waziwazi. Lakini tuliona katika mechi, mtu mmoja ndio alifanya mawasiliano na waamuzi.
 
Waombeni watu wa VAR, waombeni waje London. Mabosi wakubwa,” alisema Guardiola akiwataka wakubwa wa VAR watoe maelekezo England.
“Kilichotokea Ligi ya Mabingwa wa Ulaya msimu uliopita, bao la dakika za mwisho la Raheem ndicho ambacho kimetokea leo. Ni ngumu kukubali kwa sababu tunacheza vizuri na tunafunga bao zuri. Wao mara yao ya kwanza walipovuka nusu ya uwanja walifunga bao na la pili lilikuwa la mpira uliotulia.”
 
Back
Top Bottom