Kama kuna kitu kinamchanganya kwa sasa Pep Guardiola ni VAR. sio kama haipendi, hapana, anadai inachagua matukio. Anaishangaa na anaamini inatumika vibaya,
Juzi Jumamosi, kocha huyo wa Manchester City alishuhudia kwa mara nyingine VAR ikiinyima ushindi timu yake dhidi ya Tottenham baada ya bao la Gabriel Jesus kukataliwa katika dakika za majeruhi.