Giligiliani inawingi wa Vitamini A, B6, C,B12,pia ina wingi wa madini chuma(iron),Calcium na Magnesium, Giligiliani inasifika kwakua dawa na kinga ya magonjwa mengi
Historia inaonyesha kwamba Kiungo hiki kilitumika kama dawa tangu enzi za kale nchini Egypt.Hata hivyo,tafiti za kisayansi za karne hii ya 21 zinathibitisha taarifa hizi
Ni vyema kujua kwamba tunaposema chakula Fulani ni dawa,basi maana yake ni kwamba chakula hicho kinavirutubisho Fulani ambavyo huweza kukabiliana na ugonjwa Fulani au laa kuupa mwili uwezo wa kukabiliana na kujikinga na ugonjwa Fulani na si vinginevyo.
Hizi ni baadhi ya faida za giligiliani katika afya :
Inawezesha usagaji mzuri wa chakula mwilini,hutuliza tumbo na huondoa gesi kwenye utumbo mwembamba ambayo mara nyingi husababishwa na vyakula tunavyokula hivyo hupunguza utoaji gesi chafu (kunyampa) kwa kiasi kikubwa sana
Inapunguza cholesterol mbaya mwilin
Chanzo kizuri cha nyuzi nyuzi zinazoitajika mwilini ili kuwezesha usagaji mzuri wa chakula (Dietary fiber)
Inawafaa sana wanawake ambao hupata hedhi nzito
Huondoa chunusi na madoa kwenye ngoziUnaweza kuandaa giligiliani katika njia mbalimbali ili kuitumia kama dawa Kuondoa hedhi nzito.chemsha kijiko 1 cha chai cha mbegu za giligiliani na maji vikombe viwili.Chuja kisha ongeza sukari kidogo.
Madawa na Tiba nyingi za kisasa pia hutokana na mimea,virutubisho huvunwa kutoka kwenye mimea na vyakula na kuchanganywa na Kemikali ili kutoa vidonge na madawa ya magonjwA mbalimbali.
AVOCADO POPSICLES / LAMBA LAMBA ZA PARACHICHI NA MAZIWA : Mahitaji: Parachichi 1 kubwa kiasi 1/2 kikombe cha sukari Kopo 1 kubwa maziwa myepesi ya ( LUNA EVAPORATED MILK ) 1/2 kikombe maji Maelezo: Katika bakuli kubwa, changanya iliyosagwa parachichi, sukari,maziwa, na maji. Koroga mpaka sukari iyeyuke kabisa. Ongeza sukari zaidi kama ni lazima. Kumbuka kwamba utamu utapungua mchanganyiko ukiganda. Jaza mchanganyiko katika mifuko au vikopo na weka na vijiti katika vikopo. Gandisha katika freezer masaa 4 hadi 6. Baada ya hapo tayari kuliwa. MAZIWA YA KOPO YA LUNA YANAPATIKANA MADUKANI NA SUPER MARKETS. Enjoy πππ
MANGO ICE CREAM / LAMBA LAMBA ZA EMBE : Maembe 3 makubwa Mtindi wa vanilla au wa kawaida vikombe 5 Sukari kiasi chako Menya embe katakata vipande vidogo vidogo na mimina katika blender. Weka na Mtindi na Sukari. Saga mpaka iwe laini kabisa. Mimina mchanganyiko katika vikopo vya ice cream. Gandisha katika freezer muda wa masaa 6 au 8. Baada ya hapo lamba lamba za embe tayari kuliwa. Enjoy πππ