Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Hii inaonyesha wababe hawa wa El Clasico wamekuwa wakijali zaidi ubora kuliko uwingi ambapo katika kipindi cha miaka 10 iliyopita pale Hispania ni mara moja tu ubingwa wa La Liga uliponyoka katika mikono yao ukaenda kwa Atletico Madrid. Katika kipindi hicho wababe hao wametengeneza kiasi cha Pauni 730 milioni za mauzo.
 
Bayern Munich inashika nafasi ya 15 katika kumwaga pesa kununua wachezaji nyuma ya Arsenal, AC Milan, Roma na Monaco.

Katika klabu zote za Ulaya, Monaco ndiyo ambayo imeonekana kuwa na mbinu nzuri katika masuala ya uhamisho. Katika timu 18 za juu katika orodha hii, Monaco imeuza wachezaji kwa kiasi cha Pauni 983 milioni katika kipindi cha miaka 10 iliyopita huku ikinunua wachezaji wa kwa dau la Pauni 730 milioni.
 
Klabu za Borussia Dortmund, Sevilla na Genoa ni miongoni mwa klabu ambazo zipo katika orodha ya timu 30 bora zilizotumia pesa nyingi, lakini bila ya kutengeneza faida. Klabu mbili za Ureno, Porto na Benfica ndizo ambazo zimetengeneza faida kubwa kwa kuwanunua wachezaji kwa bei rahisi na kuwauza kwa bei ya juu. Porto ilipata Pauni 381.5 milioni na Benfica ilipata Pauni 592 milioni.
 
Hakuna klabu iliyopata faida kubwa kama Benfica ya Ureno ambayo imeuza wachezaji 29 kwa zaidi ya dau la Pauni 10 milioni na kinda mahiri, Joao Felix ameweka rekodi ya mauzo kwa kutua Atletico Madrid kwa dau la Pauni 113 milioni.

Klabu nyingine kama RB Salzburg, Sao Paulo na Basel ni miongoni mwa klabu ambazo pia zimetengeneza faida kubwa katika mauzo ya mastaa. Klabu za Kiingereza Leicester, Bournemouth, Stoke, Brighton, Aston Villa, Everton, West Ham, Wolves, Liverpool, Arsenal, Chelsea, Manchester United na City ni miongoni mwa klabu 25 za juu za Ulaya ambazo zimejikuta zikipata hasara linapokuja suala la mauzo na manunuzi.

Kwa faida ya mauzo ya wachezaji wanaoondoka, Chelsea inaongoza kwa faida baada ya kumuuza Eden Hazard kwenda Real Madrid na sasa imeuza mastaa wake kwa kiasi cha Pauni 811 milioni katika kipindi cha miaka 10 iliyopita.
 
27cae6f5-55af-44e9-a979-fe085002e125.jpeg
 
Back
Top Bottom