Hakuna klabu iliyopata faida kubwa kama Benfica ya Ureno ambayo imeuza wachezaji 29 kwa zaidi ya dau la Pauni 10 milioni na kinda mahiri, Joao Felix ameweka rekodi ya mauzo kwa kutua Atletico Madrid kwa dau la Pauni 113 milioni.
Klabu nyingine kama RB Salzburg, Sao Paulo na Basel ni miongoni mwa klabu ambazo pia zimetengeneza faida kubwa katika mauzo ya mastaa. Klabu za Kiingereza Leicester, Bournemouth, Stoke, Brighton, Aston Villa, Everton, West Ham, Wolves, Liverpool, Arsenal, Chelsea, Manchester United na City ni miongoni mwa klabu 25 za juu za Ulaya ambazo zimejikuta zikipata hasara linapokuja suala la mauzo na manunuzi.
Kwa faida ya mauzo ya wachezaji wanaoondoka, Chelsea inaongoza kwa faida baada ya kumuuza Eden Hazard kwenda Real Madrid na sasa imeuza mastaa wake kwa kiasi cha Pauni 811 milioni katika kipindi cha miaka 10 iliyopita.