Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kuna nyuzi za utata[emoji23][emoji23]
Mkuu kuna vijana wawili nimewachakata humo, maisha yao yanaumiza sana, nimewaomba kuongea nao, wakikubali nitafarijika.
Maisha ya duniani ni ya hovyo sana, pindi unapo kunywa chai wewe kuna wengine wanawaza watakula nini usiku.Mimi nanunua Kvant kwa 10,000 kuna mtu anaitafuta 5,000 akanunue unga kilo tano alishe familia. Saa hizi nimelewa mapombe yangu, kuna watoto hapo jirani matumbo yanaunguruma kwa kukosa chakula..
Nikifa kesho nitaandikiwa "RIP"?
Hapana jamani...
 
Ukiona watu unaokaa nao wanatabia za kujisemea mabaya, hali ngumu, Maisha magumu na vitu vingine kaa nao mbali. Ukiona watu unaokaa nao kazi yao ni kusema wengine vibaya kaa nao mbali. Kwasababu hayo ni mbegu unapanda ipo siku zitazaa matunda.
 
Anza kusema maneno mazuri, sema kile unachotaka kitokee na sio kile usichokitaka. Tengeneza Maisha yako kwa kuyanena vile unavyotaka yawe. Usikubali kukaa na wakatishaji tamaa au waliokata tamaa. Watu ambao wanalalamika kila kukicha, kukiwa na baridi wanalalamika, jua likiwaka wanalalamika, kukiwa na vumbi wanalalamika, kukiwa na tope wanalalamika. Usiku wanalalamika na mchana wanalalamika. Kaa nao mbali watu hawa. Kaa karibu na watu ambao wanapenda kushukuru
 
Back
Top Bottom