Fowadi huyo wa kimataifa wa Chile, ambaye ameshindwa kufanya mambo ya maana tangu alipotua Man United akitokea Arsenal Januari 2018, ameondoka kwenye kikosi hicho cha Ligi Kuu England na kwenda kujiunga na Inter Milan kwa mkopo wa msimu mzima.
Sanchez anaondoka Ole Trafford akiwa amaeifungia timu hiyo mabao matano tu katika mechi 45 alizocheza katika michuano yote, lakini akishindwa pia kucheza mechi yoyote kwenye kikosi hicho cha Kocha Ole Gunnar Solskjaer kwa msimu huu.
Muongo mmoja uliopita, supastaa Cristiano Ronaldo alipasua mioyo ya mashabiki wa Man United baada ya kuamua kutimkia Real Madrid. Ronaldo ndiye mchezaji aliyeweza kuitendea haki jezi Namba 7 huko Old Trafford na tangu alipoondoka 2009, hakuna mchezaji mwingine aliyefanya vyema akiwa na jezi hiyo maarufu.
Sanchez ni mchezaji wa tano kupewa jezi hiyo tangu Ronaldo alipoondoka, lakini gundu limemwandama, akishindwa kabisa kufurukuta na sasa amefunguliwa mlango wa kutokea huko Old Trafford, akitolewa kwa mkopo.
Wachezaji waliokuja kuvaa jezi namba 7 huko Man United baada ya Ronaldo kuondoka, wa kwanza alikuwa Michael Owen, ambaye aliishia kufunga mabao matano tu, wakati Antonio Valencia alifunga bao moja, Angel Di Maria mabao matatu, Memphis Depay mabao mawili na Sanchez mabao matatu. Mabao hayo ni kwenye Ligi Kuu England pekee. Kwa jumla Sanchez ameifungia Manchester United mabao matano tu.
Wachezaji wote waliovaa jezi namba 7 huko Man United baada ya Ronaldo kuondoka, mabao yao ya jumla waliyofunga ni 14 tu kwenye Ligi Kuu England. Hiyo ni ndani ya miaka 10.
Ndani ya muda kama huo, Ronaldo amefunga mabao 332 kwenye ligi akiwa na kikosi cha Real Madrid na Juventus (kwenye mechi 324) huku kwa ujumla wake amefunga mabao 478 katika michuano yote.
Wakati ikiwa mapema kuchukua uamuzi wa kuistafisha jezi namba 7 huko Man United, wachezaji sasa wanapaswa kuikwepa namba hiyo watakapotua Old Trafford, la sivyo yatawakuta majanga kama aliyowatokea wakali wengine kama Sanchez, Depay na Di Maria, ambao hawakumaliza misimu miwili, wakafunguliwa lango la kutokea.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.