Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Aston Villa vs Birmingham – mechi 14, kadi 59

Mara zote, Aston Villa na Birmingham City zimekutana, basi mechi zao zimekuwa za kibabe mno ndani ya uwanja. Timu hizo zimekutana mara 14 kwenye Ligi Kuu England, lakini mechi hizo zimeshuhudia kadi 59 zikionyeshwa na waamuzi, ambapo kadi za njano 57 na kadi nyekundu mbili. Hii ni moja ya mechi ambazo mashabiki wake wanafahamu shughuli inayotokea uwanjani inapopigwa. Aston Villa imerudi Ligi Kuu England msimu huu, lakini Birmingham haipo.
 
Newcastle vs Sunderland – mechi 28, kadi 139

Moja kati ya mechi za kibabe kwenye Ligi Kuu England ni ile ya Newcastle United na Sunderland. Kwa bahati mbaya, mashabiki wa ligi hiyo kwa msimu huu hawatapata uhondo huo, kwasababu Sunderland haipo kwenye ligi.

Mahasimu hao wamekutana mara 28 tu kwenye ligi, lakini kwenye mechi hizo, kadi 139 zimeonyeshwa, ambapo kadi za njano 133 na kadi nyekundu sita. Si ndani ya uwanja tu, hadi nje mechi hii ni balaa, polisi wamekuwa wakimwagwa mitaani timu hizo zinapomenyana.
 
Man City vs Man United – mechi 44, kadi 182

Hii ni Manchester derby. Manchester City inapokutana na Manchester United, basi shughuli yake ndani ya uwanja inakuwa pevu. Wababe hao kwenye Ligi Kuu England wanaopatikana katika Jiji la Manchester, kwenye mechi 44 walizokutana kwenye ligi, zimeonyeshwa kadi 182.

Si mchezo. Kwenye kadi hizo, njano ni 178 na nyekundu ni nane. Kutokana na kila timu kutaka kuwa mbabe kwa mwenzake, ndio maana wachezaji wao wamekuwa wakipigana sana buti ndani ya uwanja wanapokutana.
 
Hiyo ilikuwa ni sababu za kiusalama, kwa sababu timu vurugu zake ni balaa zinapokutana ndani na nje ya uwanja. Kwenye mechi 54 walizokutana kwenye Ligi Kuu England, zimeonyeshwa kadi 202, njano ni 186 na nyekundu 16, ikiwa ni mechi ya kibabe iliyoshuhudia kadi nyingi zaidi nyekundu kwenye ligi hiyo.
 
Chelsea vs Tottenham – mechi 54, kadi 213

London derby. Miaka ya karibuni, mechi za Chelsea na Tottenham Hotspur zimekuwa na upinzani mkali sana kutokana na wote kuwa kwenye vita ya kugombea kuwamo kwenye Top Four kukamatia tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya.
 
Arsenal vs Chelsea – mechi 54, kadi 227

Kwani Arsenal na Chelsea lini? Hivyo ndivyo mashabiki wa Ligi Kuu England wamekuwa wakiulizana mara nyingi, kwa sababu hakuna anayependa kuthubutu kukosa mechi hiyo ya kibabe. Arsenal na Chelsea wote wanaotokea kwenye Jiji la London, hivyo wanapokutana, uwanjani ni kuonyeshana ufundi na utemi.

Kwenye mechi 54 walizokutana kwenye ligi, zimeshuhudia kadi 227 zikionyeshwa, ambapo njano ni 214 na nyekundu 13. Mechi ya wanaume.
 
Arsenal vs Tottenham – mechi 54, kadi 232

Kesho Jumapili kinapigwa kitu cha maana huko Emirates. Arsenal itakuwa nyumbani kuwakaribisha mahasimu wao hao, Spurs katika mechi inayotabiriwa kuwa ya kibabe kwenye Ligi Kuu England. Mara zote, Arsenal na Spurs zinapokutana, basi shughuli huwa nzito.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…