Kinda Daniel James aliifungia United bao la kuongoza katika kipindi cha kwanza na hivyo kuwa mfungaji bora wa United mpaka sasa akiwa na mabao matatu lakini beki, Jannik Vestergaard akaisawazishia Southampton katika kipindi cha pili.
Katika dakika ya 73 ya pambano hilo, staa mpya wa Southampton, Kevin Danso alionyeshwa kadi ya pili ya njano na wakati mashabiki wa United wakiamini mastaa wao wangetumia fursa hiyo kupata bao la ushindi bado walishindwa kufanya hivyo.
Sasa Scholes anaamini timu hiyo bado ipo nyuma kiuwezeo na Solskjaer, ambaye aliwahi kutamba naye katika kikosi cha Manchester United miaka ya nyuma, analazimika kukipangua kikosi chake kwa madirisha manne yajayo.