Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kipa huyo raia wa Hispania, mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu na tayari amekataa ofa ya Pauni 350, 000 kwa wiki ili asaini mkataba mpya kwa mujibu wa mtandao wa The Sun, uliopo England.
 
MANCHESTER United ni ile ile tu. Haijabadilika. Wameanza tena maisha magumu ambayo wameyazoea katika miaka ya karibuni na mmoja kati ya watu maarufu na muhimu na klabu hiyo ametoa neno zito bila ya kuuma maneno.
Paul Scholes, staa wa zamani wa Manchester United ambaye kwa sasa ni mchambuzi wa soka pia amedai kocha wa sasa wa United, Ole Gunnar Solskjaer anahitaji madirisha matatu au manne ya usajili wa wachezaji kwa ajili ya kuifanya United ishindane tena.
United juzi Jumamosi ilikuwa katika Uwanja wa Saint Marry nyumbani kwa Southampton na ilicheza mechi yake ya tatu bila ya kuambulia ushindi baada ya kutoka sare ya 1-1 na wenyeji wao ambao walicheza pungufu kwa dakika 17.
 
Kinda Daniel James aliifungia United bao la kuongoza katika kipindi cha kwanza na hivyo kuwa mfungaji bora wa United mpaka sasa akiwa na mabao matatu lakini beki, Jannik Vestergaard akaisawazishia Southampton katika kipindi cha pili.
Katika dakika ya 73 ya pambano hilo, staa mpya wa Southampton, Kevin Danso alionyeshwa kadi ya pili ya njano na wakati mashabiki wa United wakiamini mastaa wao wangetumia fursa hiyo kupata bao la ushindi bado walishindwa kufanya hivyo.
Sasa Scholes anaamini timu hiyo bado ipo nyuma kiuwezeo na Solskjaer, ambaye aliwahi kutamba naye katika kikosi cha Manchester United miaka ya nyuma, analazimika kukipangua kikosi chake kwa madirisha manne yajayo.
 
Kwa walichokionyesha unapata hisia wanahitaji madirisha matatu au manne ya uhamisho wa wachezaji kabla ya kufikia wanapotaka kuwa,” alisema Scholes.
“United ni United. Nadhani inabidi usiipe matumaini kwa kipindi cha miaka miwili ijayo. Nadhani mpaka Ole Gunnar aondoe kila anachokitaka kitoke. Kuna madirisha manne au matano, United itaendelea kuwa nyuma ya Manchester City, Liverpool, Chelsea na Tottenham,” alisema Scholes.
 
Naye staa mwingine wa zamani wa United, Owen Hargreaves alionyesha kuwa na wasiwasi mkubwa na United baada ya timu hiyo kupoteza pointi katika mechi tatu mfululizo dhidi ya Wolves, Crystal Palace na Southampton.
“Nina wasiwasi kwa Ole Gunnar na wachezaji wake. Timu ambazo wamecheza nazo sio ngumu na wanapoteza pointi. Utakuwa msimu mgumu kwao,” alisema Hargreveas ambaye naye ameangukia katika kazi ya uchambuzi wa soka.
 
Wakati kina Scholes wakionyesha wasiwasi na kikosi cha Ole Gunnar, kocha huyo mwenyewe alidai timu yake itakuwa nzuri pindi wachezaji wakizoea mfumo mpya anaowafundisha.
“Tuna mpango uko wazi. Tunawaamini wachezaji na tunaamini jinsi tunavyofanya mambo. Unaweza kusema ni suala la muda mrefu lakini tulistahili kushinda mechi zote tatu zilizopita. Kitu ambacho hauwezi kuwa na uhakika nacho katika soka ni matokeo. Unaweza kuwa na uhakika na juhudi zao, tabia, na kile ambacho tunakifanya mazoezini. Mpaka sasa tupo katika njia sahihi. Tunafanya kazi nzuri. Tuna wachezaji wengi wazuri,” alisema Solskjaer.
 
Sasa mastaa wa United kama walivyo mastaa wa klabu mbalimbali duniani watatawanyika kwa ajili ya kupisha mechi za kimataifa na watarudi tena baada ya wiki mbili kwa ajili ya pambano gumu la nyumbani dhidi ya Leicester City.
Endapo Solskjaer atashindwa kuondoka na pointi tatu katika pambano hilo kuna uwezekano mkubwa presha ikaanza kupanda kwake na akafuata nyayo za makocha waliopita klabuni hapo baada ya kuondoka kwa Sir Alex Ferguson.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…