"Wakati naenda Arsenal kilikuwa kipindi kizuri sana, nilikuwa na furaha lakini Manchester tulikuwa tunakuwa kwa muda ule, walikuwa wananunua wachezaji ili kushinda kitu fulani ndio maana sijutii kabisa," alisema
Nadhani furaha yangu ni pale ninapocheza katika timu ya Taifa, hata Manchester nilikuwa na furaha, lakini mara kwa mara nilikuwa nawaambia marafiki zangu nahitaji kucheza zaidi," alisema.
Aliongeza sehemu ambayo anapewa nafasi ya kucheza anaonyesha makali yake, lakini kwa United alikuwa anapewa dakika 60 na mechi ijayo haanzi lakini hajui kwanini.