Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

10. Joao Cancelo – Euro 65 milioni

Manchester City waliweka mezani ofa ya mchezaji pamoja na pesa kumnasa beki wa kulia wa Juventus, Joao Cancelo. Kwenye hilo, Mbrazili Danilo alipelekwa huko Juventus huku dili hilo likimfanya Cancelo kuwa mchezaji mwenye thamani ya Euro 65 milioni na hivyo kuingia kwenye orodha ya wachezaji ghali waliosajiliwa ndani ya mwaka huu. Bado hajacheza mechi nzima Man City, ambapo alianzia benchi dhidi ya Bournemouth.
 
9. Rodri – Euro 70 milioni

Huu ni usajili mwingine wa pesa nyingi kufanywa na Manchester City wakati walipomnasa Rodri. Kiungo huyo mkabaji alinaswa kwa ada ya Euro 70 milioni kutoka Atletico Madrid. Amekuwa mchezaji ghali kunaswa na kocha Pep Guardiola kwa sababu kocha huyo siku zote amekuwa akijifikiria mara mbili mbili linapokuja suala la kutoa pesa nyingi kwa mchezaji mmoja. Tayari Rodri ameanza kuonyesha ubora mkubwa huko Etihad.
 
[emoji23][emoji23][emoji23]huyu jamaa bhana.
 
8. Frenkie de Jong – Euro 75 milioni

Barcelona walithibitisha kuinasa saini ya Frenkie de Jong kwenye dirisha la Januari, wakilipa Euro 75 milioni kupata huduma yake kutoka Ajax. Kiungo huyo bora kabisa Ulaya aliyeifikisha Ajax kwenye nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu uliopita. Tayari ameshatua Barcelona na ameshacheza kwenye mechi zote za La Liga msimu huu, huku matarajio yakiwa ni makubwa ya kufanya kweli huko Nou Camp.
 
7. Nicolas Pepe – Euro 80 milioni

Arsenal walijiingiza dakika za mwisho kwenye mbio za kumnasa winga wa Lille, Nicolas Pepe na hatimaye walifanikiwa kupata saini yake licha ya kwamba walilazimika kulipa pesa nyingi. Kocha Unai Emery aliweka rekodi ya uhamisho kwenye klabu hiyo alipolipa Euro 80 milioni kunasa saini ya Pepe. Mabao 22 na asisti 11 kwenye Ligue 1 msimu uliopita, hivyo matarajio ni makubwa kwamba atatamba sana kwenye kikosi cha Arsenal.
 
6. Lucas Hernandez – Euro 80 milioni

Staa mwingine aliyeamua kuachana na Atletico Madrid ni Lucas Hernandez. Mabingwa wa Bundesliga, Bayern Munich walivunja rekodi yao ya uhamisho wakati walipotoa Euro 80 milioni kunasa huduma ya beki huyo kwa kuvunja mkataba wake. Ameanzishwa katika mechi zote za Bundesliga ilizocheza Bayern Munich msimu huu na anaonekana kwamba atakuwa na wakati mzuri katika kikosi hicho cha Allianz Arena.
 
5. Matthijs de Ligt – Euro 85.5 milioni

Matthijs de Ligt alikuwa na msimu mzuri huko Ajax, akiwa nahodha wa kikosi hicho kilichobeba mataji ya ndani ya Uholanzi na kufika nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu uliopita. Jambo hilo lilizifanya timu nyingi kutaka saini yake ndipo Juventus walipokwenda kumnasa kwa ada ya Euro 85.5 milioni. Licha ya kwamba mwanzo wake huko Juventus si mtamu sana, lakini De Ligt hana muda mrefu kabla ya kuanza kutamba Italia.
 
4. Harry Maguire – Euro 87 milioni

Harry Maguire alitajwa mara nyingi kusakwa na Manchester United kabla ya kujiunga rasmi na timu hiyo ya Old Trafford akiweka rekodi ya kuwa beki ghali duniani. Man United walilipa Euro 87 milioni kunasa saini yake, huku wakiwapiku mahasimu wao, Manchester City kwenye kinyang’anyiro hicho. United walihitaji beki mwenye uwezo wa kuwapanga wenzake kwenye sehemu ya ulinzi na Maguire amethibitisha hilo.
 
3. Eden Hazard – Euro 100 milioni

Eden Hazard alikuwa akihusishwa na uhamisho wa kwenda Real Madrid kwa miaka kadhaa kabla ya miamba hiyo ya Hispania kufanikiwa kunasa huduma yake kwenye dirisha hili la majira ya kiangazi. Los Blancos wamenasa huduma ya Hazard kutoka Chelsea baada ya kulipa kiasi cha Euro 100 milioni, huku jambo hilo likiwafanya Real Madrid kuacha kumfukuzia Paul Pogba. Hazard bado hajaanza kucheza kutokana na kuwa majeruhi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…