Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Nitalifanyia kazi hili
Asante kwa ufafanuzi
Utafiti mpya unadai kuwa inawezekana ukosefu wa usingizi ndiyo chanzo kikuu cha kansa za aina mbalimbali. Wanasema ukilala chini ya masaa matano immune system yako inapunguza ufanisi wake wa kufanya kazi kwa asilimia 70%. Na tayari katika nchi nyingi hasa huko kwa wenzetu watu wanaofanya kazi za usiku wakiwemo walinzi, wauguzi, madaktari na wengineo wanatambuliwa kuwa wanafanya kazi hatarishi kwa afya na wanalipwa posho maalumu pamoja na kuhimizwa sana kulala kila wanapopata nafasi.
 
KIUNGO wa Real Madrid na Croatia, Luka Modric alishinda Tuzo ya Ballon d’Or kwa mwaka 2018 na hivyo kumaliza utawala wa mastaa, Cristiano Ronaldo na Lionel Messi uliodumu kwa miaka 10, walipokuwa wakibadilishana tuzo hiyohiyo.
 
Staa wake, Gerd Muller alikuwa wa kwanza kuibeba mwaka 1970. Kisha akaibeba Franz Beckenbauer, akiwa mchezaji wa pili kwenye kikosi cha Bayern, yeye akiinyakua tuzo hiyo mara mbili mwaka 1972 na 1976 na straika Karl-Heinz Rummenigge alitajwa kuwa mchezaji bora duniani mara mbili mwaka 1980 na 1981.
 
Mchezaji wa kwanza kwenye kikosi cha AC Milan kushinda tuzo alikuwa Gianni Rivera mwaka 1969, wakati Mdachi Ruud Gullit alifuatia akifanya hivyo baada ya miaka 18, 1987. Mdachi mwingine, Marco van Basten alishinda mara tatu 1988, 1989 na 1992, wakati straika wa Liberia, George Weah alinyakua tuzo mwaka 1995. Straika wa Ukraine, Andriy Shevchenko alikuwa tuzo mwaka 2004, wakati mchezaji mwisho wa Milan kunyakua tuzo alikuwa Mbrazili, Kaka mwaka 2008.
 
Juventus - mara 8

Juventus ni klabu kubwa huko Italia na imeshuhudia mastaa wake wakishinda Tuzo ya Ballon d’Or mara nane tofauti. Mtaliano, Omar Sivori alikuwa wa kwanza kubeba tuzo hiyo mwaka 1961 na kufuatiwa na Paulo Rossi, aliyekuja kubeba tuzo hiyo miaka 21 baadaye. Gwiji la Ufaransa, Michel Platini alishinda tuzo hiyo kwa miaka mitatu mfululizo kati ya 1983 na 1985, wakati Roberto Baggio aliibeba mwaka 1993.
 
Barcelona - mara 11

Barcelona imekabana koo na Wahispaniola wenzao, Real Madrid kwenye kubeba tuzo hiyo ya Ballon d’Or. Mhispaniola, Luis Enrique alikuwa wa kwanza kubeba tuzo hiyo akiwa na Barcelona mwaka 1960, kisha gwiji, Johan Cryuff alikuja kuibeba kwa miaka miwili mfululizo 1973 na 1974.
 
Ilisubiri kwa miaka 20 kisha ikashinda tena kupitia kwa straika wa Bulgaria, Hristo Stoichkov mwaka 1994, wakati Rivaldo alikuja kuibeba miaka minne baadaye. Ronaldinho naye alibeba tuzo mwaka 2005 na baada ya hapo, Lionel Messi alionyesha ufalme kwenye timu hiyo akibeba mara tano na kufikisha idadi ya mara 11 kwa klabu hiyo ya Barcelona.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…