Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

dc299e74-305b-443a-9b9b-c0ff484b2a63.jpeg
 
MAGOLI MENGI KUWAHI KUFUNGWA NA GOLI KIPA

Kazi ya goli kipa katika timu ni moja tu nayo ni kulinda goli lake ili kuzuia wapinzani wasifunge.Lakini pale golikipa anapojiongezea kazi ingine ya pili siku zote lazima liwe jambo la kusataajabisha sana,
 
Mkongwe mmoja ambaye ni raia wa Brazili ambaye naye kipindi chake alikuwa ni goli kipa aliishangaza dunia kwa kuweka rekodi ambayo mpaka kupinduka kwa dunia labda ndio kutaifanya rekodi iyo ivunjwe.
 
Rogerio Ceni ndie mlinda mlango aliyewai kufunga magoli mengi kuliko magoli kipa wote kuwai kutoa, ambapo anashikilia rekodi ya kufunga jumla ya magoli 131. Mlinda mlango huyo ndie anayeongoza kutimiza kazi ambayo haimuhusu yeye akiwa kama goli kipa ambapo alikuwa akitimiza kazi iliyopaswa kufanya na mshambuliaji.
 
Kipindi hicho akiwa anaichezea klabu ya Sao Paulo ya nchini kwao Brazili ambapo klabu hiyo ndiyo aliitendea kazi akiwa kama kocha baada ya kustaafu anatazamwa kuwa kipa hatari kuanzia katika majukumu yake kama kipa na kama mshambuliaji pia. Kipa anayemfata kwa kufunga magoli mengi ni Jose Luis Chilavert akiwa na magoli 71,magoli 60 nyuma ya R.Ceni.
 
MCHEZAJI ALIYEFUNGA MAGOLI MENGI KATIKA HISTORIA YA SOKA


Tukizungumzia maswala ya magoli wengi katika vichwa vyetu yanatujia majina makubwa kama Pelle, Ronaldo na Eusebio au hata Messi hawakaribii hata kidogo ukija katika swala la upachikaji magoli au kucheka na nyavu kama wanasoka wanavyopenda kusema.
 
MECHI ILIYOHUDHULIWA NA MASHABIKI WENGI ZAIDI TANGU KUGUNDULIWA KWA SOKA DUNIANI.

Katika fainali ya kombe la dunia ya mwaka 1950 katika ya Brazili na uruguay iliyofanyika katika viwanja vya amerika kusini ndiyo mechi inayoripotiwa kuhudhuriwa kwa miaka mingi zaidi duniani.
 
Mechi hiyo iliyopewa kwa jina "huge upset" ndiyo iliyohudhuriwa zaidi ambao mauzo rasmi ya tiketi yanaripotiwa kuwa 173,850 lakini waandishi wengi wanasema kuwa uwanjani kulikuwa na watu zaidi ya 210,000.
 
MAGOLI MENGI KUFUNGWA KATIKA MECHI MOJA
Amini usiamini, hii ndio haitokuja hata kukalibiwa kuja kuvunjwa, naamini hivyo maana ni rekodi ya aina yake. Ilikuwa mwezi oktoba mwaka 2002 katika mchezo kati ya AS Adema dhidi ya SO I'Emyrne ambapo walicheza mchezo wa kuwania ubingwa na mchezo huo kuisha kwa mabao 149-0.
 
Ilikuwa hivi, huko nchini Madagascar ambapo kulikuwa na mchezo wa kugombania ubingwa ambapo kwa sheria za michuano hiyo timu zinatakiwa kucheza nyumbani na ugenini katika mchezo wa fainali ambapo katika mchezo wa kwanza ambapo SO I'Emyrne ilikuwa nyumbani ikiikaribisha AS Adema na mchezo huo kuisha kwa sare ya 2-2. Lakini wachezaji wa timu iliyo nyumbani yaani Emyrne hawakulizishwa na maamuzi ya mwamuzi wa mchezo huo. Ambapo katika mchezo wa marudiano ili atakayeshinda hapo yatajumlishwa matokeo ya nyumbani na ugenini kisha mshindi kupatikana.
 
Lakini mchezo huo ulipoanza Emyrne ambao safari hii walikuwa ugenini wakaamua kuanza kujifunga wenyewe wakiamini kwa kuwa mwamuzi aliamua kuwakatili mchezo wa kwanza tena wakiwa nyumbani basi hata huu hawawezi kushinda kwa vili "mcheza kwao hutunzwa"
 
Back
Top Bottom