Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

lianaalexandra___Buof6uUgKCu___.jpg
 
SIMULIZI; VYAKWAKO UNALIA BARAZANI WENZAKO WANALIA CHUMBANI! Kijana mmoja alille kwa shida na Mama yake, alimuona namna ambavyo alikua akihangaika na yeye pamoja na waodgo zake. Kila mara alipowaona watoto wa Shangazi zake na Baba zake wadogo wakiishi maisha ya raha aliumia na kumuuliza Mungu ni kwanini alimchukua mapema Baba yake. Mara nyingi alisikia stori za namna Baba yake alikua na pesa na namna ambavyo walikua na maisha mazuri. Kuna wakati alimlaumu Mama yake kwa kuchezea Pesa za Baba yake, akijua kuwa Baba yake alaicha utajiri mwingi, lakini kwakua alimuona namna Mama yake alikua akihangaika basi alitulia na kumuonea huruma. Kulelewa na Mama yake na wote kufanya kazi kwa pamoja na ndugu zake kulimfanya kuwapenda sana ndugu zake, aliwaamini kwa kila kitu hata alipopata kazi na kuwa na pesa. Alimchukua Mama yake na ndugu zake, walikua wakiishi pamoja. Baada ya kuoa na kupata watoto bado aliendelea kuwapenda ndugu zake, aliwaamini zaidi na kuwashirikisha katika mambo yake. Kila aliponunua kiwanja aliandika jina la Mama yake na kuwashirikisha ndugu zake, hakumuambia mkewe, lakini alishangaa kila mara mkewe alikua anajua mambo yake. Mkewe alikua akijua mali zake zote na kila mara kumtaka kuandika majina yao wote, alikasirika kwani alihisi labda mkewe alikua anamfuatilia na alitaka kumdhulumu. Siku moja alinunua Shamba kubwa, hakumuambia mtu yeyote zaidi ya Mama yake, lakini siku iliyofuata mkewe alimuuliza kuhusu lile Shamba, alikasirika na kumuuliza alijuaje, alitaka kumpiga mkewe lakini Mama yake alifika na kuingilia kati. Aliwaulza nini tatizo ndipo alimuambia mkewe anamfuatilia sana, anamchunguza na anataka kumtapeli, alimuuliza kwanini ndipo alipomuambia kuhusu Shamba. “Sijamuambia mtu yeyote ziadi yako Mama sasa yeye kajuaje?” Kijana aliuliza kwa hasira, lakini Mama yake alimtuliza na kumuambia mimi ndiyo nimemuambia. Kijana alishangaa kwani kila sikua alidhani Mama yake yuko upande wake.
 
Alimshutumu Mama yake kwa kumsaliti. “Mama wewe pekee ndiyo nilikua nakuamini, unajua namna ulivyopata shida na sisi sasa kwanini hutaki kuniunga mkono unanisaliti!” Aliongea kwa hasira, Mama yake alimuangalia, huku akitabasamu alimuambia. “Nimefanya hivyo kwakua nakupenda Mwanangu, sitaki wanao waje kuishi kwa shida kama ulivyoishi wewe!” Kijana alishangaa hakumuelewa Mama yake. “Baba yako alikua kama wewe, hakuniamini hivyo aliamini ndugu zake zaidi, walikua wanapendana na kama wewe aliandika mali zote majina ya Mama yake. Lakini alipokufa ndugu zake walitutenga, upendo ulipotea na shetani aliingia, waliwasahu nyinyi watoto wa Marehemu na kwakua mali zote zilikua kwa majina ya Mama yake basi nyinyi hamkupata chochote kwani kisheria mali za Baba yenu hazikua zake.” Mama alitulia, kijana alibaki kaduwaa. “Mwanangu najua unanipenda na unapenda wadogo zako, lakini kamwe sitaruhusu wanao wateseke kama mlivyoteseka nyinyi, ukifa leo mali ulizoziacha hazitakua za mkeo wala wanao, zitakua ni za kwangu kwakua umeandika majina yangu…” “Lakini Mama mimi nakuamini huwezi kuwadhulumu wanangu.” Kijana alijaribu kumuelimisha Mama yake. “Nikweli siwezi kuwadhulumu lakini kumbuka wewe si mtoto wangu pekee hivyo kama ukiacha mali kwa majina yangu, siku na mimi nikifa basi zitachukuliwa na wanangu wengine. Wanao hawatarithi kwakua kisheria si wanangu ni wajukuu hivyo hawatapata chochote. Hicho ndicho kilichotokea baada ya Baba yako kufariki. Bibi yenu hakuwatenga lakini naye hakuishi sana. Alipofariki tu mali zote zake zilienda kwa wanae, Baba yako alishafariki hivyo asingerithi na nyie mlikua wajukuu hivyo hamkupata chochote ingawa mali zote zilikua za Baba yenu. Hivyo huo utajiri wote uliokua ukiuzisia kwa watu kua Baba yenu anao uliishia kwa ndugu zake mimi sikuambulia kitu. Ndiyo Maana ulipokua unaniandikia mali zako majina yangu nilijua unataka kuiangamiza familia yako.
 
Kila kitu nilibadilisha na kuandika majina ya wanao, hata kama humuamini mkeo lakini wanao ndiyo wana haki ya mali zako si mimi wala hawa ndugu zako, nawapenda lakini nafahamu binadamu walivyo, kama huamini angalia Shangazi zako na Baba zako wadogo nao walikua familia na Baba yako kama wewe na wadogo zako lakini ni lini walikuja hata kuwanunulia kiatu cha Shule?” Kijana alibaki kimya hana chakusema, alimuangalia Mama yake kwa mshangao, Mama yake likua akimaanisha. Mama yake aliondoka na kuwaacha pale, aliingia ndani na kutoa nyaraka zote alizokua akipewa na mwanae wakati akiandikishwa mali, alimuonyesha na zote alikua ameandika majina ya wajukuu zake. Aliwakabidhi na kuwaambia “Acheni ujinga sasa hivi nyie mna watoto walindeni nyie kama wazazi na si kusubiri ulimwengu uwaadhibu! Mke wako huyu anaweza kukusaliti na kuchukuliwa na mwanaume mwingine lakini kamwe hatawasaliti watoto wake, mimi ni Mama najua kua ninaweza kufanya kitu chochote kwaajili ya wanangu, hata ukiniachia hizi mali siku mwanangu mwingine akipata shida nitamsaidia nazo hata kamka najua si zake!” Kijana alipokea kwa aibu, alimuangalia mke wake ambaye alikua kakasirika kwani aliona namna ambavyo mumewe hakua akimuamini. Kichwani bado alikua haamini kuwa ndugu zake wanaweza kumsaliti, Mama yake alimuangalia na kumsoma, ni kama alikua anajua alichokua akiwaza, alimuuliza “Huniamini, hivi unajua ndugu yako naye anajenga?” kijana aliduwaa alikua hajui kitu. “Haya baki hivyo hivyo vyakwako unalia Sebuleni wenzako wanalia Chumbani!” Mama yake aliongea huku akiondoka kamuacha mdomo wazi!
 
Back
Top Bottom