SIMULIZI; VYAKWAKO UNALIA BARAZANI WENZAKO WANALIA CHUMBANI! Kijana mmoja alille kwa shida na Mama yake, alimuona namna ambavyo alikua akihangaika na yeye pamoja na waodgo zake. Kila mara alipowaona watoto wa Shangazi zake na Baba zake wadogo wakiishi maisha ya raha aliumia na kumuuliza Mungu ni kwanini alimchukua mapema Baba yake. Mara nyingi alisikia stori za namna Baba yake alikua na pesa na namna ambavyo walikua na maisha mazuri. Kuna wakati alimlaumu Mama yake kwa kuchezea Pesa za Baba yake, akijua kuwa Baba yake alaicha utajiri mwingi, lakini kwakua alimuona namna Mama yake alikua akihangaika basi alitulia na kumuonea huruma. Kulelewa na Mama yake na wote kufanya kazi kwa pamoja na ndugu zake kulimfanya kuwapenda sana ndugu zake, aliwaamini kwa kila kitu hata alipopata kazi na kuwa na pesa. Alimchukua Mama yake na ndugu zake, walikua wakiishi pamoja. Baada ya kuoa na kupata watoto bado aliendelea kuwapenda ndugu zake, aliwaamini zaidi na kuwashirikisha katika mambo yake. Kila aliponunua kiwanja aliandika jina la Mama yake na kuwashirikisha ndugu zake, hakumuambia mkewe, lakini alishangaa kila mara mkewe alikua anajua mambo yake. Mkewe alikua akijua mali zake zote na kila mara kumtaka kuandika majina yao wote, alikasirika kwani alihisi labda mkewe alikua anamfuatilia na alitaka kumdhulumu. Siku moja alinunua Shamba kubwa, hakumuambia mtu yeyote zaidi ya Mama yake, lakini siku iliyofuata mkewe alimuuliza kuhusu lile Shamba, alikasirika na kumuuliza alijuaje, alitaka kumpiga mkewe lakini Mama yake alifika na kuingilia kati. Aliwaulza nini tatizo ndipo alimuambia mkewe anamfuatilia sana, anamchunguza na anataka kumtapeli, alimuuliza kwanini ndipo alipomuambia kuhusu Shamba. “Sijamuambia mtu yeyote ziadi yako Mama sasa yeye kajuaje?” Kijana aliuliza kwa hasira, lakini Mama yake alimtuliza na kumuambia mimi ndiyo nimemuambia. Kijana alishangaa kwani kila sikua alidhani Mama yake yuko upande wake.