Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Hivyo tafuta kujiamini wewe mwenyewe na jithamini kwa sababu wewe ni wa thamani na hii ni muhimu katika maisha yako na siri moja nikuambie mambo yote hayo yanatoka ndani mwako kisha ukishaweza kuyaonyesha kwa wenzako au marafiki zako hizo likes zitakuja wala hutaziomba.
 
hutahitaji kubustiwa na mtu kwa maneno ndio upate nguvu siku akikosekana utaumia na pia utaishi maisha yenye malengo yasiyoendeshwa na wengine maana kama unajithamini una nguvu na una malengo na unaamini una thamani hutapata shida utafanya chochote hata kama dunia yote itakupinga hii ndio nguvu ya ushindi kwako wala sio likes nyingi na shares utakazopata maana hata hawajui malengo yako ila wanaogopa kukuangusha na wanafanya kwa unafiki kwa kuiongopea nafsi yako nawe unaridhiki maana uliwaambia wasipofanya watakuwa vilaza!
 
Njia za kusaidia ili uweze kujipenda, kujithamini na kujiamini

Rafiki nimeshakueleza hapo juu kuwa kujipenda na kujiaminini sio kazi ndogo ila kuna siri kubwa nayo nimeshaieleza hapo juu ila nairudia tena hapa ni kwamba siri hii huanzia ndani ya nafsi yako nayale tunayoyaona nje ni matokeo yake pale utakapofanya vitu vikubwa na ukawashangaza watu nao watavutitiwa nawe na kuanza kukupenda tu bila hata kuwaambia neno moja. Basi sasa hebu tuangalie njia hizi za kuongeza kujiamini, kujipenda na kujithamini mwenyewe kwanza;
 
Ukitaka kuwa mkamilifu lazima utakwazika au kukutana na vikwazo hapa lazima utakata tamaa kwa sababu lengo lako ni kupendwa na si vinginevyo lakini kama huna lengo la kupendwa lakini unaamini kuwa hakuna aliekamilika na ukaendelea kufanya yaliyobora kwa kujiamini, juhudi, na kujithamini hakika lazima watu watakubali tu kazi yako hata wale walioikataa mwanzo na kuitoipenda kabisa.
 
Saidia wengine katika jamii kwenye mambo mbali mbali.
Ukisaidia wengine katika jamii lazima utapendwa tu kwa sababu utakuwa ni msaada kwa watu. Umewasaidia kufikia kitu fulani au jambo fulani hivyo imekuwa tunu kwao kwa nini wasikupende? Hii ni kanuni ya asili hata kama hutataka kupendwa lazima utapendwa kwa sababu umejitengenezea thamani na kwa kawaida kitu chenye thamani hupendwa.
 
Zipo kazi nyingi za kijamii ambazo unaweza ukafanya mfano kama wewe ni Mkristo siku za jumamosi nenda kasaidie hata kusafisha nyumba za ibada au kama kuna siku maalumu ya kufanya hivyo wasaidie wahusika na kazi zingine nyingi. Nafikiri unaona kama maajabu lakini inawezekana fanya utaona maajabu yake.
 
Kuwa na afya njema na muonekano mzuri.
Hapa nafikiri hakuna ubishi, mtu mwenye muonekano mzuri wenye staha kwanza anajiamini, anajipenda na anajithamini. Mtu huyu huwa kivutio kwa wengine nao humpenda kwa sababu anajijali kwanza yeye kwa nini wengine wasimjali? Kila kitu kinaanza na wewe mwenyewe wala hakuna miujiza ya mbinguni hapa!
 
Hapa unahitaji uanzie na afya yako kula mlo mzuri utaowezesha mwili wako kuwa na nguvu za kutosha (sio za kupigana namaanisha kiafya), fanya mazoezi kuweka mwili wako vizuri uwe na mvuto hapa hutaonekana una umbo zuri tu bali utajisikia vizuri pia. Kama kuna vyakula unaona sio vizuri kwa afya yako (zingatia ushauri wa wataalamu wa afya) anza kuviacha taratibu ili kulinda afya ambayo ikiharibika itaharibu muonekano wako.
 
Hali kama hizi ukikutana nazo usiendekeze mawazo hasi kama ‘kila siku mimi tu sijui kwa nini…’, ‘mimi sifai…’ na maswali mengine ambayo yatachangia kujishusha tafadhali epukana nayo badala yake weka fikra chanya, kwa mfano kama umeachwa na mwenzi unaweza ukajiambia nitapata mwingine bora zaidi ya Yule… hii itasaidia kurejesha kujiamini kwako na thamani yako.
 
Jishughulishe na kile unachoweza kukifanya vizuri zaidi
Kila mmoja anajua kuwa anaweza kufanya nini kwa ustadi zaidi. Sasa hapa jali hicho kitu chako wala usijilinganishe na wengine kwa sababu hata wao hawawezi kufanya unachoweza wewe hivyo wewe ni wa kipekee na usijilinganishe nao,
 
Jishughulishe na kile unachoweza kukifanya vizuri zaidi
Kila mmoja anajua kuwa anaweza kufanya nini kwa ustadi zaidi. Sasa hapa jali hicho kitu chako wala usijilinganishe na wengine kwa sababu hata wao hawawezi kufanya unachoweza wewe hivyo wewe ni wa kipekee na usijilinganishe nao,
 
hali hii ya kujilinganisha itakufanya uanze kujiona hufai ila wao ndo wanaweza, wakati ukweli ni kwamba kila mmoja ni mjuzi kwenye eneo lake hivyo fanya chako kwa ustadi hata waengine watavutiwa na watakupenda wewe zaidi.
 
Back
Top Bottom