Katika maisha kila mtu ana ndoto ama kiu ya mafanikio lakini si wote wanafanikiwa kufikia ndoto/kiu zao(yao) ya mafanikio kwa sababu mbalimbali ambazo huwarudisha nyuma au kuwakwamisha kufikia hitaji lao maishani.
Kwanza kabisa hebu tuangalie maana ya malengo ni nini? Kwa maana rahisi kabisa malengo ni mipango ambayo umeweka kwa ajili ya kutimiza/kufikia kitu fulani katika muda ujao.
Hivyo basi kama tulivyoona maana ya Malengo; kumbe Malengo ni kama ramani inayoonyesha jinsi ya kufikia mipango mbalimbali tuliyojiwekea kwa muda fulani.
Kitu muhimu rafiki ninachopenda kukumbusha hapa ni kwamba ukiweka malengo jitahidi kuyaheshimu kwani usipoyaheshimu hutayatimiza hatimae utayaweka kando na hutayatimiza kwani utakuwa na visingio au sababu lukuki za kutofikia malengo ilhali unatambua fika kuwa ni ramani na dira ya mafanikio yako.
Kwa leo naomba niishie hapo hadi wakati mwingine tena lakini kitu muhimu kabisa katika kufikia mafanikio ni malengo! Hivyo nakuomba uzinduke ili kufikia mafanikio.