Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Sifa za Banda Bora la Kuku
Ili mfugaji afanikiwe na apate faida anayoitegemea ni lazima awe na banda bora la kufugia kuku wawe wa kisasa au wa kienyeji. Sio kila banda linalojengwa ni bora kwahiyo ni lazima mahitaji halisi yazingatiwe ili ufugaji uweze kutoa matokeo bora yanayotarajiwa na mfugaji.
 
Hewa na mwanga: Kama walivyo viumbe wengine wote, kuku wanahitaji hewa safi na mwanga wa kutosha kwahiyo banda lao lazima liwe na mambo. Ukubwa wa madirisha ya kuingiza hewa unategemea mahali banda lilipo, kama ni sehemu yenye joto inabidi yawe makubwa na kama ni sehemu ya baridi madirisha yasiwe makubwa sana. Jaribu kuzuia upepo mkali kuingia ndani ya banda la kuku ama sivyo kuku wataugua ugonjwa wa mafua na niumonia na vifaranga vinaweza kufa kwa ugonjwa wa baridi
 
Mgawanyo bandani: Banda bora inabidi liwe na sehemu tofauti kwa ajili ya stegi mbalimbali za ukuaji, sehemu ya vifaranga ambayo inatakiwa kuwa na joto sahihi kwa ajili ya ukuaji wa vifaranga na mwanga, sehemu ya kuku wakubwa ambao wanahitaji joto la kawaida ambapo kuku wa nyama na mayai inabidi watenganishwe na watu wengi huwa wanasahau chumba cha kuku wagonjwa. Ili kuepusha maambukizi, kuku wenye magonjwa ambukizi inabidi watengwe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…