Jinsi ya kuandaa:
-Pika wali kisha uache upoe au tumia kiporo.
-Andaa vipande vya nyama ya kuku visivyokuwa na mifupa.
-Changanya vipande vya kuku na pilipili manga, bizari na chumvi. Changanya hadi uwiano uwe sawa.
-Weka sufuria jikoni kisha kaanga nyama ya kuku hadi iwe ya kahawia. Ikiiva, weka pembeni na funika vizuri isipoe.
-Bandika sufuria jikoni weka kitunguu maji, kitunguu saumu, njegere zilizochemshwa, pilipili hoho, green beans na carrot. Geuza geuza kwa muda wa dakika 2.
-Pasua mayai, mwagia kwenye sufuria kisha koroga haraka haraka ili vichanganyike na yaive vizuri.
-Ongeza wali koroga ili kuchanganya vizuri, weka kuku, endelea kukoroga takribani dakika 2 hadi 3.
-Ongeza soy sause kwenye chakula, koroga vizuri ichanganyikane na chakula mpaka maji maji yakauke kwenye chakula na wali uwe na rangi ya kahawia.
-Pakua chakula na ukipambe uwezavyo tayari kwa kuliwa.