Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Matokeo yake imani na mitazamo hasi juu ya watu wenye imani zingine imepelekea kuwepo kwa chuki na visasi baina ya jamii au watu wenye imani tofauti, vita na mauaji; hii ni kutaka kuleta usawa wa kiimani kwa mabavu, watu wamepoteza wapendwa wao katika kupigania au kutetea imani – hii athari kubwa sana.
 
Pia watu badala ya kufanya shughuli za uzalishaji wameendekeza mapambano ya kiimani yaliyotawaliwa na mitazamo na hisia zao, hatimaye wanasababisha ulimwengu kuwa na maumivu makubwa na kuufanya usiwe sehemu salama ya kuishi tena tofauti na hapo awali wakati maisha yanaanza ilivyokuwa.
 
Chakufanya endelea na mambo yako bila shaka unafaidika nayo ndio maana muda mwingine unakuwa upo tayari kuitetea ila fahamu tu kuwa haitawezekana wote mkubaliane jambo hilo kama nilivyoeleza awali kuwa sisi ni wanadamu na tuna akili na fikra tofauti hivyo kuwa na mawazo au fikra zinazofanana haitakuja tokea na hata kama ikitokea ni muda mchache sana ambapo mbeleni mtatofautiana tena na mtaanza tena malumbano ambayo yatapelekea kupoteza muda, kuchukiana, kugombana na wakati mwingine husababisha vita na mauaji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…