Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

FB_IMG_1569660855034.jpeg
 
Dhana ya kujitambua kwa zama za sasa imekuwa kama kengele ya kanisa au azana ya msikiti, kwa jinsi ambavyo hutamkwa mara kwa mara.Sasa yatosha kwa jinsi tulivyoisikia,leo nataka tuje na kitu kipya kama kilivyoelezwa katika kichwa cha mada yetu.
Sipendi kukuchukulia muda wako naomba niingie moja kwa moja kwenye mada
 
PIMA UMRI NA KIWANGO CHA FIKRA ZAKO

Sote tunafahamu kuwa hakuna kiwango maalumu cha kufikiri kilichoidhinishwa kimataifa kutoka umri mmoja na mwingine. Bali tunaviwango vya kimataifa vinavyotoa uwiano wa umri wa mtoto na kuandikishwa shule.Hata hivyo kuna uwezekano mkubwa wa kupima kiwango cha fikra zako kwa kulinganisha na umri wako.
 
Unaweza kupima fikra zako kwa kutazama ubora wa matokeo ya kila unachoamua kutenda pasipo kusaidiwa na mtu mwingine.Pia unaweza kupima fikra zako kwa kuzilinganisha na ubora wa fikra za watu wenye kiwango cha juu cha fikra katika umri wako. Lakini mwisho wa yote viwango bora kabisa vya kifikra vinalenga juu ya usahii wa wakati katika kutekeleza jambo fulani.
 
Unaweza kupima jinsi unavyopanga,unavyoamua,unavyotekeleza, na kuendelea au kusitisha maswala fulani fulani katika maisha yako na aina ya matokeo unayoyapata kwa kuzingatia ubora wake.
Kwa kufanya hivyo itakusaidia kuanza kupata picha ya namna gani unajitambua.
 
TAFUTA KUJUA UPEKEE ULIONAO

Hii nayo ni kati ya mbinu bora inayokufanya ujitambue.Watu wengi hupenda kufanana na watu fulani fulani haswa watu ambao wao huwaita role model (mtu wa mfano),Na kusahau kuwa yeye ndiye role model na.1 kwake binafsi.Makosa haya humpelekea mtu huyo kujua zaidi kuhusu huyo role model na.2 na upekee wake kuliko anavyoweza kujifahamu mwenyewe.
 
Leo imekuwa ni kawaida kumsikia mtu akieleza kwa ufasaa upekee alionao OBAMA na MKEWE lakini ukimuuliza upekee alionao akakujibu kirahisi tuu sijui.Kitu pekee kitakachokuokoa na tatizo hili ni kuamua kufahamu upekee ulionao na si upekee wa mtu mwingine au Role model wako.
 
TAFUTA KUJUA CHANGAMOTO ZINAZOKUKABILI

Kama kweli umedhamiria kujitambua unatakiwa kufahamu changamoto au matatizo yanayokukabili.Changamoto hizo zinaweza kuwa ni zile zinazotokana na rika ,mazingira ,kiwango cha elimu yako,Hali uliyonayo (ulemavu, mahitaji maalumu au uathirika wa magonjwa,ndoa,bila ndoasingle nk. ).
 
Kama ni rika tambua rika lako linakabiliwa na changamoto zipi.Ikiwa ni mazingira tafuta kujua changamoto za kimazingira ulizonazo.Unaishi kijijini ,mjini,shuleni,chuoni,mfanyakazi,kiongozi,mfuasi au vinginevyo ,jiulize katika mazingira hayo unakabiliwa na changamoto gani. Inawezekana wewe ni teenager (13-19 miaka) au kijana au mzee, jiulize kuhusu changamoto zako.Vivyo hivyo kwa kiwango cha elimu pamoja na hali kama ilivyofafanuliwa katika maban😵rodhesha changamoto zinazokukabili
 
Kumbuka hata uonevu wa kibinadamu wa kawaida hutokea zaidi kwa watu wasiozingatia kipengele hiki cha ufahamu wa changamoto. Hakikisha unafahamu wapi utakwama kabla hujafikia na kuanza kuchukua hatua mapema iwezekanavyo.kitendo hicho kitakufanya uwe macho saa zote na kila atakayekuona atakuthamini hivyo kutokuwa na madhara kwako.
 
Back
Top Bottom