Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

TAFUTA KUJUA WAJIBU NA MAJUKUMU YA WATU WA RIKA LAKO

Kwa haraka unaweza kufikiri kuwa nataka kufundisha uraia.Utanisamehe kama nitakuwa nimekukumbusha kitu unachoimba au ulichoimba kilasiku shuleni.Lengo langu nataka nikufumbue macho kuhusu wajibu na majukumu kama dhana muhimu katika kujitambua.
 
Mfano; mama mmoja alikuwa akilia kwa uchungu nje ya nyumba yake huku akijitupatupa chini na kugalagala.Majirani wakaja mbio na kukusanyika kufahamu kilichotokea.Lakini kila walipomuuliza mama alichokua akililia aliwaonyesha kidole katika mlango uliokuwa wazi.
 
Watu wakakimbilia ndani na kumkuta mtoto wa miaka minne na nusu aliyewekewa kila kikorokoro cha kuchezea lakini hakuna alichokishika wala kukichezea. Walipotoka na kumuuliza mama mbona hatukuona chochote zaidi ya mtoto na vitu,mama akaongeza kilio na kusema “masikini mwanangu asala gani hii! huyu ni mwanangu watatu ,wenzake waliotangulia walikufa kwa moto shambani kwasababu hawakuweza kusogea hata hatua moja moto ulipotokea nilipokuwa kisimani kuteka maji.kinachoniumiza zaidi ni kuona hata huyu naye hagusi chochote nilichomwekea nahisi naye atakufa kifo kama cha wenzake
 
Kwa mfano huo tunapata picha ya mtu asiyetambua wajibu wake anavyoweza kuleta hasara kubwa kwake yeye mwenyewe ,kwa familia yake na kwa taifa lake.Mama aligundua kuwa mtoto wake hajitambui kwa kutonyanyua chochote.majukumu ya msingi ya mtoto wa umri ule ni kucheza.Kutokucheza ilikuwa ni ishara tosha ya kutokujitambua.
Jiulize kama wewe ni mmoja wa wale wasiowajibika?.
 
Piga picha na kuyatazama majukumu yako kama mtoto,kijana,au mzee.
Jiulize kuwa wewe ni Yule mtoto mwenye kila kilicho mbele yake lakini hakuna anachogusa?.
Jiulize kuwa umekuwa mtu wa kunyooshea vidole majukumu au umekuwa mstari wa mbele kutumikia?.
Umewahi kushiriki kutatua kero yeyote nyumbani kwako ,mtaani kwako au maeneo yaliyokuzunguka?
Jiulize unafanya nini katika kujiandaa kutumia fursa zinazojitokeza duniani?
Nafasi uliyonayo unaitumia kufanya wengine kuinuka au unawadidimiza?
Jiulize kama wewe ukikosekana duniani, dunia itakuwa imepata hasara yeyote?
 
Wakati unajiuliza maswali hayo ni wazi kuwa utaanza kupata picha ya jinsi ulivyo kwa kupima uwajibikaji wako.Kitendo kicho kitakufanya uongeze uelewa wako juu yako binafsi na kwasababu hiyo utaingia kwenye kundi la watu wanaojitambua.
 
PIMA KUJIAMINI KWAKO
Ili kujitambua inakupasa kuchukua jukumu hili msingi la kupima kujiamini kwako.Hebu jichukue katika fikra zako na kujiweka mbele ya umati mkubwa wa watu wenye uelewa wa kutosha.Jaribu kuwaelezea au kuonyesha kitu ambacho unakifahamu kwa usahihi kabisa hapa duniani.Unahisi unaweza kukifanya kikamilifu bila hofu wala kubabaika.
 
Unaweza kujikumbusha mambo ambayo yalikuwa yanakufanya ushindwe kujiamini kama bado yapo au la.
Pima ubora wa unachofanya kama una nafasi yeyote katika viwango vya kidunia?.
Kama wewe unajihusisha na sanaa je sanaa yako inaweza kumvutia mtu yeyote duniani?.
kama ni huduma je! huduma yako inaweza kumfaa mtu yeyote duniani?
Kama ni mwanafunzi je wewe unaweza kuwa mwanafunzi bora popote duniani au ni hapo kijijini kwako tu?.
Unaweza kushindanishwa na mtu yeyote duniani kwa hilo ambalo wewe ni bora sana hapo kwenu au ubora huo ni wa hapo kwenu tu?.

Kwa vipimo hivyo vitakufanya uzidi kujitambua na kuchukua hatua ya kuondosha mapungufu uliyonayo na kukufanya uzidi kujiamini
 
WEKA VIPINDI MAALUMU VYA KUJITATHIMINI
Kitendo cha kujitathimini kitakufanya kujichunguza na kujiweka karibu na wewe binafsi.Tatizo kubwa tulilonalo leo duniani ni kwamba tunawatu wengi ambao wako karibu sana na watu wengine lakini hawako karibu na wao wenyewe. Kifupi ni kwamba wanajua sana kinachoendelea kwa watu wengine kuliko kinachoendelea kwao binafsi.
 
Wanalaumu watu hawana elimu wakati wenyewe hawana,
Wanatetea unyanyasaji wa kijinsia wakati wao wenyewe wananyanyaswa,
Wanalaumu watu wanaovunja ndoa wakati wao wenyewe wana nyumba ndogo,
Wanalaumu kuhusu wizi wa viongozi wa umma wakati Wao mwenyewe wanaiba kwenye kampuni zao.
 
Sasa,kitu ambacho kinaweza kusaidia katika kujitambua ni kufanya tathmini binafsi juu ya mwenendo wako.Kabla hatujaanza kukosoa uzembe wa watu wengine tenga vipindi maalumu ikiwa ni kila baada ya wiki,mwezi au mwaka kutathimini ni uzembe wa namna gani umefanya na matokeo yake.Hata hivyo unaweza kufanya tathimini za kila siku ili kutokuwa na mlundikoano wa tafakuri za muda mrefu kuhusu namna ulivyoishi.
 
Unaweza kutathimini kiwango cha mafanikio kwa kulinganisha na matarajio,kiwango cha mapungufu kwa kwa kulinganisha na namna ulivyoshindwa.Kama mafanikio hayakufikia malengo basi ni wazi kuwa bidii na mbinu bora zaidi zinahitajika na kama matokeo ni kushindwa basi ni wazi kuwa mfumo mzima wa maisha inabidi ubadilike na mbinu mpya zinatakiwa.
 
.Kila baada ya tathimini lazima uje na mapendekezo mapya yenye mbinu mpya ,mikakati mipya na matarajio mapya.Kwa kufanya hivyo ni dhahili kuwa kiwango chako cha kujitambua kitakua na kuongeza mabadiliko ya kila siku katika maisha yako.
 
KUBALI KUANZA UPYA

Bila kujali wasifu ulionao unaweza kuonyesha kiwango cha kujitambua kwako kwa kuanza upya mara tu unapobaini kuwa kunamakosa makubwa katika mwenendo wa maisha yako.mtu mwenye kiwango cha chini kabisa cha kujitambua hawezi kuanza upya .kwasababu ya kutojitambua kwake haoni shida kwa lolote limpatalo na kuhisi kuwa amestahili.
 
Mtu asiyejitambua haoni umuhimu wa kubadilisha mtindo wa maisha kwasababu hufikiri kuwa kufanya hivyo ni sawa na kupoteza wakati.Inashangaza sana kumwona mtu anatumia staili ya aina moja katika kupambana na changamoto ambazo kila siku zinabadilika.
 
Jenga tabia ya kukubali kuanza upya kila unapoona kuwa hatua ya kiwango cha makosa ulichofikia hakiwezi kurekebishika.mfano ,kama pengine fani unayoitumikia haiendani kabisa na kipaji ulichonacho kubali kuanza kujifunza fani nyingine.Na endapo marafiki ulionao wanakusababisha kushindwa kutimiza majukumu yako, kubali kuanza kutafuta marafiki wapya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…