Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

*Maelekezo*
🔹Andaa vitunguu saumu, tangawizi na ndimu.
🔹Tenga kitunguu saumu kwenye sehemu mbili.
🔹Osha na kisha marinate samaki wako – weka tangawizi, vitunguu saumu, ndimu na chumvi.
🔹Acha samaki akae kiasi – ikiwezekana kwenye jokofu – ili viungo viingie vizuri.
🔹Menya vitunguu, nyanya, pilipili hoho na karoti na kisha kata vipande vidogo.
🔹Weka mafuta kwenye kikaangio kilicho jikoni. Subiria yapate moto vizuri.
🔹Weka samaki na ukaange hadi aive vizuri. Ukimaliza weka samaki pembeni.
🔹Bandika sufuria, weka mafuta uliyokaangia samaki. Subiria yapate moto vizuri kisha weka vitunguu na uvikaange mpaka viwe vya kahawia.
 
Weka pilipili hoho na koroga mchanganyiko.
Weka vitunguu saumu huku ukiendelea kukoroga kuzuia visigande kwenye sufuria.
Weka karoti na endela kukoroga
🔹Weka nyanya kisha funika kwa muda wa dakika 5. Hakikisha kuwa moto si mkali sana, bali uwe wa wastani.
🔹Kamulia ndimu kwenye mchanganyiko na weka chumvi kisha koroga kiasi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…