Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi tayari
IMG-20190930-WA0022.jpeg
 
Kwa mtazamo wa haraka haraka unaweza kufikiria kuwa hakuna njia ya kukabiliana na msongo wa mawazo kwa sababu hata iweje bili za umeme na maji zitazidi kuja, siku ndiyo ile ile ya saa 24 na kazi za kufanya zinazidi kuwa nyingi na majukumu ya familia yatazidi kuongezeka
 
Kubaini Vyanzo Vya Msongo Wa Mawazo



Hatua ya kwanza kabisa ni kubaini vyanzo vya msongo wa mawazo katika maisha yako. Kazi hii siyo rahisi sana kwa sababu vyanzo hivi huwa sio vya wazi na ni rahisi kudharau mawazo, hisia na tabia ambavyo huwa ndiyo mwanzo wa kukupa msongo wa mawazo. Kwa mfano, unawezajua fika kuwa mara nyingi huwa upo katika wasiwasi mkubwa wa kukamilisha kazi ulizopangiwa katika muda uliopewa, lakini usijue kuwa tabia yako ya kuahirisha kazi ndiyo tatizo na si ukubwa wa kazi unazopewa.
 
Kubaini ni nini vyanzo vya msongo wa mawazo kwako, chunguza kwa ukaribu sana tabia, mwenendo na visingizio vyako. Kama hutokubali kuwa wewe mwenyewe ni mhusika katika kusababisha na kuvilea vitu vinavyokuletea msongo wa mawazo (Stressors), itakuwa vigumu sana kupambana na tatizo lako la kuwa na msongo wa mawazo.
 
Andaa kijitabu kubaini ni nini kinakuletea msongo wa mawazo na vipi huwa unakabiliana na hali hiyo. Kila wakati utakapopatwa na msongo wa mawazo, fuatilia kwa kutumia kijitabu chako. Ukifanya hivyo kila siku, utajifunza ni mambo gani yanakusumbua na yanavyohusiana. Katika kijitabu chako andika yafuatayo:
 
Back
Top Bottom