Katika siku nzuri kwa Arsenal, Rob Holding, Kieran Tierney na Hector Bellerin, ambaye alikuwa nahodha, wote walicheza dakika 90 na kuendeleza kurejea kwao uwanjani baada ya kuuguza majeraha.
Mtu mmoja amekiri katika mahakama ya London jana Alhamisi kuwa alijaribu kuwapora nyota wawili wa Arsenal, Mesut Ozil na Sead Kolasinac katikati ya mwaka huu.
Alifikishwa mbele ya mahakama ya Snaresbrook Crown kwa kuunganishwa kwa video na kukiri alijaribu kumpora Ozil, mwenye umri wa miaka 30 na ambaye alitwaa Kombe la Dunia akiwa na Ujerumani, na Kolasinac, 26.
Alifikishwa mbele ya mahakama ya Snaresbrook Crown kwa kuunganishwa kwa video na kukiri alijaribu kumpora Ozil, mwenye umri wa miaka 30 na ambaye alitwaa Kombe la Dunia akiwa na Ujerumani, na Kolasinac, 26.
Picha za video za tukio hilo zinamuonyesha beki huyo wa Bosnia aliyejiunga na Arsenal mwaka 2017, akiwafukuza watu wawili ambao walivaa kofia ngumu na nguo nyeusi.
Wachezaji hao wawili walikosa mechi za mwanzo za msimu huu kutokana na jaribio hilo la kuporwa kutokana na wasiwasi wa usalama wao, lakini tayari wamesharejea kwenye timu yao ya Arsenal.
Lille "Wanacheka tu wakiichungulia akaunti yao ya benki ilivyonona” linapokuja suala la uhamisho wa Nicolas Pepe, amesema Martin Keown, huku Arsenal wakiaminika kuwa wamelipa pesa nyingi kuliko thamani halisi ya mchezaji huyo anayecheza chini ya kiwango waliyemnunua kwa Pauni 72 milioni.
Arsenal waliweka rekodi binafsi ya uhamisho walipomsajili winga huyo wa Ivory Coast na kuwa mchezaji ghali zaidi katika historia ya klabu hiyo ya London katika dirisha la uhamisho lililopita.
Pepe, 24, alitua kwa mbwembwe Emirates Stadium, akitajwa kugombewa na klabu nyingi kubwa za Ulaya.
Mambo makubwa yalitarajiwa London Kaskazini, lakini winga huyo kishada amekwama kufikia wakati huu.